Noe Mawaggali
Noe Mawaggali (+ Mityana 31 Mei 1886) ni mfiadini mmojawapo kati ya Wakristo 22 wa Kanisa Katoliki wanaojulikana na kuheshimiwa duniani kote kama Wafiadini wa Uganda.
Hao walikuwa wahudumu wa ikulu ya kabaka wa Buganda Mwanga II (1884 - 1903) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na kardinali Charles Lavigerie.
Noe, akikataa kishujaa kukimbia dhuluma, alitoa kwa hiari kifua chake kichomwe na askari kwa mikuki yao. Kisha kuchomwa, alitundikwa kwenye mti hadi alipotoa roho yake kwa kumpenda Yesu.
Hawa ndio wafiadini wa kwanza wa Kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu.
Pamoja na wenzake alitangazwa na Papa Benedikto XV kuwa wenye heri tarehe 6 Juni 1920, halafu na Papa Paulo VI kuwa mtakatifu tarehe 18 Oktoba 1964 huko Roma.
Sikukuu yao huadhimishwa tarehe 3 Juni, lakini ya kwake mwenyewe tarehe 31 Mei[1].
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |