Wamisionari wa Afrika

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Charles Martial Lavigerie, mwanzilishi wa shirika la kimisionari la White Fathers

Wamisionari wa Afrika (kirefu Wamisionari wa Bibi Yetu wa Afrika, kifupi zaidi M. Afr.) ni jina rasmi la shirika la kimisionari linalojulikana kwa Kiingereza kama "White Fathers" (kwa Kifaransa "Pères Blancs"), kutokana na rangi ya kanzu yao.

Lilianzisha mwaka 1868 na Charles Martial Lavigerie, askofu mkuu wa kwanza wa Algiers, Aljeria, ambaye baadaye akawa kardinali.

Lengo lilikuwa hasa uinjilishaji wa bara la Afrika, na kweli wanashirika walijitosa kufanya kazi kubwa ambayo inaendelea hata leo, ambapo lina mapadri kama 1,500.

Kisheria leo ni shirika la maisha ya kitume la Kanisa Katoliki.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

ChristianitySymbol.PNG Makala hii kuhusu dini ya Ukristo bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wamisionari wa Afrika kama historia yake, matokeo au athari zake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.