Nkhotakota

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mwaya Beach katika Nkhotakota Bay kwenye Ziwa Nyasa
Eneo la Wilaya ya Nkhotakota
Nkhotakota

Nkhotakota (zamani Kota Kota; jina linalotokana na lugha ya Chichewa kwa ajili ya "kona kona") ni mji na makao makuu ya Wilaya ya Nkhotakota katika Kanda ya Kati, Malawi. Kufikia mwaka 2018, Nkhotakota ilikuwa na idadi ya wakazi waliokadiriwa kuwa 28,350.

Mji huo uko kwenye mwambao wa Ziwa Nyasa (huko huitwa Ziwa Malawi) ikiwa ni mojawapo ya bandari kuu kwenye ziwa hilo.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Nkhotakota iko kwenye mwinuko wa mita 472 kwenye mwambao wa Ziwa Malawi. [1] Iko kwenye ukingo wa miamba unaotazamana bandari ya asili iliyoundwa na kisiwa cha mchanga . [1]

Nkhotakota iko umbali wa kilomita 200 kutoka Lilongwe, mji mkuu wa Malawi, na kilomita 378 kutoka Blantyre, jiji kubwa zaidi la Malawi. [2]

Historia[hariri | hariri chanzo]

Katika karne ya 19 Nkhotakota ilikuwa kundi la vijiji vilivyotumika kama soko la wafanyabiashara wa watumwa. Waafrika mbalimbali walikutana hapa na Waswahili kutoka mwambao wa Bahari Hindi na Waarabu.[3]

Mmisionari David Livingstone alitembelea mji mara mbili kwenye miaka 1861 na 1864 na kuleta taarifa juu ya ubaya wa biashara ya watumwa hadi Ulaya. Kuna miti miwili inayokumbukwa kama "Livingstone tree" ambako anasemekana alijadiliana na mkuu wa Waarabu Salim bin Abdullah [4]. Baadaye rais wa Malawi Hastings Banda alitoa hotuba chini ya mti mwingine huko Nkhotakota katika miaka ya 1960, huu unaojulikana kama Mti wa Livingstone. [4] Mji huu ulikumbwa na mafuriko ya mwaka 2001, na ulikuwa eneo lililoathiriwa zaidi katika eneo la Kati la Malawi. [5] Leo, Nkhotakota ndio mji mkubwa wa kitamaduni wa Kiafrika nchini Malawi [1] na una ushawishi mkubwa wa Waswahili-Waarabu. [6]

Usafiri[hariri | hariri chanzo]

Nkhotakota ni mojawapo ya bandari kuu kwenye Ziwa Nyasa, [7] ikihudumiwa na kivuko cha MV Ilala ambacho huvuka ziwa kila wiki. Uwanja wa ndege wa karibu uko Kasungu kwa umbali wa km 77. Mabasi hutumia masaa 2 kutoka Salima. [8] Aidha, mabasi madogo yanatoka hapa hadi Nkhata Bay kando ya barabara kuu inayounganisha miji hii. [9]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 "Nkhotakota". Encyclopædia Britannica. 2008. Iliwekwa mnamo 27 June 2008.  Check date values in: |accessdate= (help)
  2. "Malawi distance table". Wild Malawi. 2008. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 8 September 2008. Iliwekwa mnamo 20 June 2008.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  3. "Nkhotakota". Encyclopædia Britannica. 2008. Iliwekwa mnamo 27 June 2008.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. 4.0 4.1 Murphy, Alan; Armstrong, Kate; Firestone, Matthew D.; Fitzpatrick, Mary (2007). Lonely Planet Southern Africa: Join the Safari. Lonely Planet. uk. 197. ISBN 1-74059-745-1. 
  5. "More Rains, Renewed Problems". AllAfrica. 21 March 2001. Iliwekwa mnamo 1 July 2008.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  6. Murphy, p. 159.
  7. "Malawi: Transportation". Encyclopædia Britannica. Iliwekwa mnamo 27 June 2008.  Check date values in: |accessdate= (help)
  8. Murphy, p. 176.
  9. Murphy, p. 191.