Nenda kwa yaliyomo

Nikolasi wa Myra

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Nikola wa Myra)
Nikolasi wa Myra jinsi alivyochorwa na mtawa Mrusi katika karne ya 12.

Nikolasi wa Myra (Mtakatifu Nikolasi kwa Kigiriki Ἅγιος Νικόλαος agios nikolaos; 2706 Desemba 343),[1][2] alikuwa askofu wa mji wa Myra akaendelea kuwa mmoja wa watakatifu maarufu zaidi wa Kanisa la Kikristo.

Tarehe 6 Desemba ni sikukuu yake[3] inayosheherekewa na Wakristo Wakatoliki, Waorthodoksi na pia na sehemu ya Waprotestanti katika Ulaya ya kati na kaskazini.

Hakuna habari nyingi za kihistoria zenye uhakika juu ya maisha yake lakini hadithi zilizosimuliwa juu yake ziko tele.

Myra leo hii inaitwa Demre, ni mji kusini mwa Uturuki, si mbali na Antalya. Ulikuwa mji wa bandari.

Nikolasi alikuwa na sifa ya kutenda miujiza pamoja na uponyaji.

Anasemekana alikuwa na tabia ya kuwaletea watu maskini na watoto zawadi kwa siri; kwa hiyo hukumbukwa hadi leo kwenye sikukuu yake ambako watoto katika nchi mbalimbali hupokea zawadi zinazowekwa ndani ya viatu au ndani ya soksi.

Kutokana na desturi hii amekuwa pia kielelezo au chanzo cha Baba Krismasi iliyo desturi badala ya Nikolasi.

Katika Ulaya ya karne za kati aliheshimiwa kama mtakatifu msimamizi wa wanabahari na wafanyabiashara; hapo ni sababu mojawapo ya kwamba kuna makanisa mengi sana yenye jina lake.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. "Who is St. Nicholas?". St. Nicholas Center. Iliwekwa mnamo 7 Desemba 2010.
  2. "St. Nicholas". Orthodox America. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2011-09-07. Iliwekwa mnamo 7 Desemba 2010.
  3. Martyrologium Romanum
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.