Nenda kwa yaliyomo

Muhinda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Muhinda ni kata ya Wilaya ya Buhigwe katika Mkoa wa Kigoma, Tanzania.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa kuwa 10,366 [1].Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 18,211 waishio humo.[2] Ilikuwa na wakazi wapatao 28,550, hata kuzidi makao makuu ya wilaya ya Buhigwe kwa mujibu wa sensa ya mwaka 2002.

Hii ni kata inayopatikana eneo la Manyovu kutokea Kigoma Mjini, barabara ya Mwandiga-Manyovu ambapo kumeanzishwa Wilaya ya Manyovu-Buhigwe barabara ya Munanila-Kasulu mjini.

Kata ya Muhinda tangu ukoloni ina vijiji vipatavyo vinne: Muhinda, Mwayaya, Nyaruboza na Mbaga.

Kijiji cha Muhinda, makao makuu ya kata, kimegawanywa kama ifuatavyo: Muhinda, Kigaraga, Ruhuba na Kikelenke, kila eneo likiwa mtaa mkubwa wenye shule ya msingi na nyingine mbili ni sekondari: St. Bakanja na Muhinda Secondary.

Eneo hili limo kati ya kanda za mvua nyingi muda wote wa kipindi cha masika. Ni eneo la kiikwetolio katika Afrika.

Kilimo chake kikuu ni kahawa, migomba, nanasi, chikichi, mahindi, mihogo, mtama, uwele, maharagwe, njegere na misitu minene ya mbao. Pia kuna ufugaji wa ng'ombe, nguruwe na kuku.

Kilimo cha kahawa ni maarufu eneo zima la Manyovu, vikiwemo Kalinzi, Mkabogo, Matyazo, Muhinda, Mwayaya, Munanila, Nyakimwe, Kitambuka, Kibwigwa, Mukigo, Nyarubanda. Wenyeji hupaita Kalinzi "Chalinze, Mbeya, Arusha, Bukoba au Kilimanjaro ya Manyovu Buhigwe".

Biashara ni hasa ya mbao na kahawa, vile kuna wafanyabiashara katika soko la kata Muhinda.

Dini kuu ni mbili, Ukristo na Uislamu, nazo zinamwabudu Mwumba wa mbingu na dunia, Mungu wa kweli wa wanadamu wote. Ukristo ndio wenye asilimia kubwa, kwani kuna Ukatoliki, Anglikana, Waadventista Wasabato, Wapentekoste (PAG, TAG, EAGT, PEFA, FPTC), Moravian n.k. Kata ina kanisa kubwa la Kikatoliki la Mt. Maria Mlango wa Mbingu tangu mwaka 1946. Uislamu una Wasuni, Washia na Wahabia.

Kata za Wilaya ya Buhigwe - Mkoa wa Kigoma - Tanzania

Biharu | Buhigwe | Bukuba | Janda | Kajana | Kibande | Kibwigwa | Kilelema | Kinazi | Mkatanga | Mubanga | Mugera | Muhinda | Munanila | Munyegera | Munzeze | Muyama | Mwayaya | Nyamugali | Rusaba

Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Kigoma bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Muhinda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.