Malouma
Malouma | |
Amezaliwa | Mauritania |
---|---|
Nchi | Mauritania |
Kazi yake | Msanii na Mwanasiasa |
[[Picha:|300px|thumb|Malouma jukwaani mwaka 2004]]
Malouma Mint El Meidah (kwa Kiarabu: المعلومة منت الميداح, pia Maalouma au Malouma; * 1 Oktoba 1960) ni mwimbaji, mtunzi wa nyimbo na mwanasiasa nchini Mauritania. Kisha kuzaliwa katika familia ya waimbaji, alipokuwa na miaka 12 alishiriki mara ya kwanza katika tamasha ya uimbaji. Baada ya kipindi cha kupumzika uimbaji wake kutokana na kuolewa na mume aliyemkataa alirudi kwenye jukwaa.
Tangu miaka ya 1990 aliingia katika siasa akipigania demokrasia. Tangu mwaka 2007 amechaguliwa na kurudishwa kama mbunge wa senati.
Ametunga nyimbo nyingi pamoja na muziki na kushiriki kwenye tamasha za kimataifa.
Familia
[hariri | hariri chanzo]Alizaliwa 1 Oktoba 1960 katika mji mdogo wa Mederdra katika Mauritania kusini magharibi. Familia yake ilikuwa ya waimbaji na wanamuziki, hivyo alifundishwa tangu utotoni kuimba na kutumia ala za muziki. Pamoja na kusikiliza muziki wa kimapokeo wa Kiberber, alipenda pia uimbaji wa Kiarabu kama nyimbo za Umm Kalthoum au Fairuz. Alipokua alianza kuvutwa pia na muziki wa blues.
Uimbaji
[hariri | hariri chanzo]Aliandika wimbo wa kwanza alipokuwa na umri wa miaka 16 "Habibi Habeytou" (Mpenzi wangu, nilimpenda). Humo alikosolea kawaida ya wanaume kuwafukuza wake katika nyumba wakipata mke mpya kijana. Wimbo huu ulimletea umaarufu lakini alishambuliwa pia na wengine. Baadaye alihamia pamoja na familia yake kwenye mji mkuu Nouakchott ili apate nafasi pana zaidi kwa muziki wake.
Lakini katika mazingira ya kuongozwa na mapokeo aliolewa na kuacha tamasha hadi mwisho wa miaka ya 1980.
Mwaka 1988 aliimba kwenye tamasha ya Karthago huko Tunis. Katiba nyimbo zake aligusa masuala kama umaskini, magonjwa, na uhuru wa maoni. Kuanzia hapo alionyeshwa pia kwenye vituo vya runinga vya nchi za Kiarabu. Nyumbani kwake alikataliwa sasa kuwa na tamasha au nyimbo zake kurushwa kwenye runinga au redio.[1]
Wakati huo Malouma alianza kushiriki katika siasa akajiunga na chama cha upinzani kilichodai mwisho wa udikteta. Baada ya kukataliwa kwenye media za Mauretania pia albamu yake ya kimataifa ilipigwa marufuku mwaka 1998, lakini vijana walimpenda.
Hatimaye mwaka 2003 kulitokea maandamano ya wananchi 10,000 mjini Nouakchott waliodai uhuru kwa uimbaji wake na rais Ould Taya alimkubali.[2]
Siasa
[hariri | hariri chanzo]Mwaka 2007 Mauretania iliona uchaguzi huru wa kwanza wa historia yake na Malouma alichaguliwa kuwa mbunge wa senati akiwa mmoja wa wanawake sita kati ya maseneta 56[3]. Serikali mpya ilipopinduliwa na wanajeshi mwaka 2008, Malouma alitunga nyimbo za kupinga uasi huu akakamatwa. Katika uchaguzi uliofuata akarudishwa kwenye senati upande wa upinzani.
Mwaka 2014 Malouma aliachana na upinzani akahamia upande wa chama cha serikali.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ All about Maalouma Ilihifadhiwa 30 Januari 2016 kwenye Wayback Machine., Malouma and the Sahel Hawl Blues, Teacher resource guide, University Musical Society, University of Michigan, Ann Arbour 04/05
- ↑ Malouma, la chanteuse du peuple Ilihifadhiwa 23 Septemba 2017 kwenye Wayback Machine. UMS University of Michigan Musical Society, Teacher Resource Guide, 04/05
- ↑ "المعلومة بنت الميداح.. ألحان الفن وأحلام السياسة". Al Jazeera (in Arabic). Doha, Qatar: Al Jazeera Encyclopedia. 12 February 2014. Retrieved 16 January 2016.
Viungo vya Nje
[hariri | hariri chanzo]- Malouma in concert (video)
- Malouma, profile and interview (video)
- Fondation Malouma Ilihifadhiwa 1 Agosti 2015 kwenye Wayback Machine. (in French)
- Malouma, Mauritania's Biggest Musical Export Ilihifadhiwa 15 Februari 2016 kwenye Wayback Machine. (2010 audio produced by Global Notes)
- Paintings created by Sidi Yahya to illustrate Malouma's album Knou