Makari Mkuu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Picha takatifu ya Mt. Makari Mkuu.

Makari Mkuu (300 hivi - 391) alikuwa mkaapweke na padri wa Misri.

Tangu kale anaheshimiwa na Waorthodoksi wa Mashariki, Waorthodoksi na Wakatoliki kama mtakatifu.

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe 15 Januari, 19 Januari[1] na 4 Aprili kadiri ya madhehebu.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Mt. Makari Mkuu akisimama karibu na Kerubi.

Mzaliwa wa Misri Kusini, aliwahi kufanya biashara ya chumvi, akaoa, lakini mke wake akafa mapema.

Mwaka 330 hivi akawa mfuasi wa Antoni Mkuu jangwani.

Huko alikataa upadrisho akahamia pengine aliposingiziwa vibaya.

Hapo alihamia kwenye jumuia ya bonde la Sketes (leo Wadi El Natrun) alipokubali kupewa upadri na kuwa kiongozi wa kiroho wa wamonaki. Kati ya wanafunzi wake wa miaka 356-384 kuna Sisoe, Isaya, Aio, Mose Mwethiopia, Pafnusi, Zakaria, Teodoro wa Ferme.

Hivyo monasteri yake ilichangia sana ustawi wa umonaki ikadumu hai hadi leo.

Miaka 373-375 askofu Mwario Lusio wa Aleksandria alimpeleka uhamishoni kwa imani yake.

Kama alivyowafundisha wengine, aliishi kwa Mungu tu katika sala, akajulikana kwa hekima yake.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo kwa Kiswahili[hariri | hariri chanzo]

  • Misemo ya Mababa wa Jangwani (Apophthegmata Patrum) – tafsiri ya W. Ngowi, O.F.M.Cap. – ed. Salvatorianum – Morogoro 2000ISBN 0-264-66350-0

Marejeo mengine[hariri | hariri chanzo]

  • Maloney, GA, SJ (trans.), 1992, Pseudo-Macarius. The Fifty Spiritual Homilies and the Great Letter, CWS, New York: Paulist Press
  • Mason, AJ (trans.), 1921, Fifty Spiritual Homilies of St Macarius the Egyptian, London: SPCK
  • Plested, Marcus, 2004. The Macarian Legacy: The Place of Macarius-Symeon in the Eastern Christian Tradition. Oxford: OUP

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.