Majadiliano ya mtumiaji:Kisare
Karibu kwenye Wikipedia kwa Kiswahili!
Tunamfurahia kila mmoja anayeingia na kuungana nasi. Hii ni kamusi elezo ya maandishi huru. Unaweza kuandika makala uipendayo ama kuitafsiri kutoka Wikipedia ya lugha nyingine.
Ukipenda kutumia kurasa zetu za mwongozo na msaada, a) ukitumia simu bofya kwa "Dawati" chini kwenye dirisha lako na b) ubadilishe mwonekano wa Wikipedia kwa kubofya "Switch to old look" kwenye menyu upande wa kushoto.
Kwa mawili matatu labda tazama:
- Kuhusu ukurasa wako wa mtumiaji na kurasa nyingine
- Ukurasa wa mwongozo
- Jamii:Msaada (makala zilizomo humo zinaweza kusaidia mara nyingi)
- Ukurasa wa jumuia (pamoja na Wikipedia:Wakabidhi, penye majina walio tayari kukusaidia)
- Makala za msingi za Wikipedia
Jisikie huru kuuliza swali lolote lihusianalo na Wikipedia hii. Karibu kujitambulisha kwenye "Ukurasa wa mtumiaji". Ukitaka kupata kwanza uzoefu wa kuweza kuhariri Wikipedia, tafadhali tumia ukurasa wako kwa majaribio. Humo unaruhusiwa kujipatia uzoefu wa uundaji wa makala za Wikipedia! Juu yako mwenyewe uandike tu kwenye ukurasa wako wa mtumiaji. Humo uko huru kutangaza chochote upendacho, kama si biashara au matusi.
Ujue miiko:
- usilete kamwe matini wala picha kutoka tovuti za nje.
- usiingize matangazo ya kibiashara (pamoja na kuelekeza kwa kurasa zenye matangazo).
- usimwage kamwe matini kutoka google-translate au programu za kutafsiri.
- usitumie kama vyanzo vya taarifa au tanbihi <ref>Wikipedia (au mradi mwingine wa Wikimedia)</ref>, ila unaweza kutumia vyanzo vyake kwa kuvitaja vyenyewe moja kwa moja.
Tunakushauri pia kuandikisha email yako; haitaonekana na wengine lakini wataweza kukuandikia kupitia mfumo wa Wikipedia. Karibu sana!
Welcome to Kiswahili Wikipedia!
We welcome you even if you don't speak Kiswahili. For a bot flag go to this site. If you try to edit entries as a non-speaker, it is better to first communicate with one of our admins who can advise you. You may find them at Wikipedia:Wakabidhi. And, please:
- do not post computer translated texts (like Google Translate, Content Translation, etc. all do not work for Swahili)
- nor copied texts/images from other webs to this site!
- do not use links to commercial pages, never post anything that looks like advertising.
- do not use as references <ref>Wikipedia (or another project of Wikimedia)</ref>, though you can use their references by writing them themselves.
As a newcomer we advise that you register your email. This will not be visible to others but it allows us to notify you, which often is helpful in case of problems.
Anuary Rajabu (majadiliano) 11:02, 28 Machi 2023 (UTC)
Kuhusu Jamii na Mbegu
[hariri chanzo]Salamu ndugu Kisare,hongera kwa kuwa mwana Astronomia,nimeona umefanya hariri katika makala kadhaa,na kuondoaa jamii,ni vyema kama jamii unataka kuongeza jamii fulani yenye mahusiano na makala fulani,ni heri kuongeza jamii mpya kuliko kutoa jamii iliyokuwepo, na katika kuweka mbegu, si vyema kutoa mbegu iliyopo bila ya kuweka kigezo kingine cha mbegu,Amani sana Idd ninga (majadiliano) 13:31, 21 Septemba 2023 (UTC)
- Salamu,kwanini huwa unaondoa mbegu katika makala za Astronomia na baada ya hapo unaacha bila ya kuweka kigezo chochote cha Mbegu ?, Idd ninga (majadiliano) 11:47, 23 Septemba 2023 (UTC)
- Karibu makala zote za astronomia zilikuwa na kigezo cha Wikinyota. Katika kigezo hiki, kuna jamii ya Astronomia. Kwa hivyo, makala zote hizo zilionekana katika jamii ya astronomia pamoja na vijamii vyake, na jamii ya astronomia ilikuwa na mparaganyo mwingi. Siwezi kuhariri kigezo kwa sababu ukarasa wa kigezo ulifungwa. Nilikuwa nitafanya vigezo vengine ili visitoe jamii ya astronomia kwa kujiendesha. Nimeshafanya mwanzo wa hiyo. Kwa mfano, nilifanya kigezo cha Makundinyota (Constellations). Kisare (majadiliano) 19:24, 23 Septemba 2023 (UTC)
- Pia, sijaondoa kigezo cha mbegu cha makala zozote Kisare (majadiliano) 19:32, 23 Septemba 2023 (UTC)
- Karibu makala zote za astronomia zilikuwa na kigezo cha Wikinyota. Katika kigezo hiki, kuna jamii ya Astronomia. Kwa hivyo, makala zote hizo zilionekana katika jamii ya astronomia pamoja na vijamii vyake, na jamii ya astronomia ilikuwa na mparaganyo mwingi. Siwezi kuhariri kigezo kwa sababu ukarasa wa kigezo ulifungwa. Nilikuwa nitafanya vigezo vengine ili visitoe jamii ya astronomia kwa kujiendesha. Nimeshafanya mwanzo wa hiyo. Kwa mfano, nilifanya kigezo cha Makundinyota (Constellations). Kisare (majadiliano) 19:24, 23 Septemba 2023 (UTC)
Hongera kwa kugusa makala za elimuanga
[hariri chanzo]Pamoja na pongezi, hizo ni kazi za mpendwa wetu marehemu Ingo Koll (Kipala). Tusingependa kuona urithi wake ukitapanywa. Unaweza kuwasiliana na wakabidhi kupitia ukurasa wa jumuia. Ili upate usaidizi zaidi... Karibu sana! Muddyb Mwanaharakati Longa 19:25, 21 Septemba 2023 (UTC)
- Asante sana kwa kunikaribisha katika jumuiya hii :) Kisare (majadiliano) 23:14, 21 Septemba 2023 (UTC)
Sayari ndogo
[hariri chanzo]Umeanzisha makala na jamii zenye kichwa hicho, lakini ni tupu. Vipi? Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 06:57, 23 Septemba 2023 (UTC)
- Samahani, ninapanga kuandika makala hii. "sayari ndogo" (minor planet) ni aina inayotia ndani sayari kibete, asteroidi, na violwa vingine vidogo vya mfumo wa jua. Hapakuwa na makala ya "sayari ndogo" kwa hivyo nilitaka kuiandika lakini sikuwa na wakati. wikendi hii nitaandika kidogo. Amani sana Kisare (majadiliano) 18:32, 23 Septemba 2023 (UTC)
Majira
[hariri chanzo]Ndugu, kama hujaishi Afrika, pengine ni vigumu kwako kuelewa majira yetu. Ni tofauti na yale ya Ulaya na Marekani... Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 14:40, 4 Machi 2024 (UTC)
- Naelewa kwamba majira katika maeneo yaliyopo mbali na ikweta ni tofauti na yale ya maeneo ya kaskazini zaidi… Lakini kuna marejeo mengi yanayoleta “vuli” na “masika” kama majina ya “autumn” na “spring”, hata kama vuli na masika kwa asili ni majina ya majira ya mvua ndogondogo na majira ya mvua nyingi. Kisare (majadiliano) 19:24, 4 Machi 2024 (UTC)
Mahoré
[hariri chanzo]Ndugu, umerudisha tena jina la Kiingereza Maore kwa kisiwa cha Ufaransa ambacho kwa Kifaransa kinaitwa Mahoré (au Grande-Terre). Unapoona nimekataa badilisho lako fulani, badala ya kulilazimisha tena, ingefaa uniulize sababu. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 11:24, 16 Machi 2024 (UTC)
- Kwa Kiingereza ni Maore, kwa Kifaransa ni Mahoré, lakini kwa Kimaore (lugha ya Maore iliyo lahaja ya Kikomori kinachohusiana sana na Kiswahili) na Kiswahili ni Maore. Kwa hivyo nilibadilisha jina la ukurasa huo. Hata ukurasa wa Kimaore unatumia tahajia hii. Kisare (majadiliano) 12:15, 16 Machi 2024 (UTC)
Majina ya nchi
[hariri chanzo]Ndugu, unaendelea kubadilisha majina ya nchi bila kuwasiliana na yeyote na bila kujali kwamba kurasa nyingi zana zinatumia la awali, hasa jamii. Angalia tu: [[jamii:watu wa Algeria]]. Hii inasumbua sana. Kwanza tujadiliane na wakabidhi wengine, halafu tutekeleze kwa kubadilisha kurasa zote walau za jamii. Ukiendelea hivi itanibidi kukusimamisha kwanza, ingawa michango yako mingine ni mizuri. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:54, 22 Machi 2024 (UTC)
Majedwali za nchi
[hariri chanzo]Ndugu, nimejaribu kufungua ukurasa juu ya Marekani nikaona jedwali halionekani. Labda ni hivi kwa kurasa nyingine pia. Vipi? --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:24, 7 Aprili 2024 (UTC)
- Kigezo cha jedwali la nchi kilivunjika kwa sababu kiliumbwa kikiwa na makosa sana. Kwa hivyo nimekitengeneza kigezo na ninatengeneza makala zilizo na kigezo hicho. Kisare (majadiliano) 04:49, 8 Aprili 2024 (UTC)
- Pia kutengeneza makosa ya kigezo na kukiboresha kulisababisha makala zenye kigezo hicho kuwa tupu, kwa sababu kigezo sasa kina maingizo mapya. Kisare (majadiliano) 05:21, 8 Aprili 2024 (UTC)
- Asante kwa jibu. Ungekuwa na ustaarabu huo kila mara tungeshirikiana vizuri zaidi. Bahati mbaya pengine unaonyesha dharau kwetu wa Wikipedia ya Kiswahili. Amani kwako!
Ushoga
[hariri chanzo]Ndugu, umebadilisha sana ukurasa juu ya ushoga, tena, kama kawaida yako, bila mawasiliano. Wewe unaishi Marekani na sisi Tanzania. Kumbuka hilo. Hatuko tayari kuvumilia ubeberu wenu katika masuala nyeti kama hili. Sisi tumeshajadiliana na kuona hatuwezi kuunga mkono mambo kama hayo. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:24, 7 Aprili 2024 (UTC)
- Ndugu, wewe ni mzungu mwitalia, "sisi" ni nani? Ukurasa huo una taarifa kosefu sana, k.m. kuchanganya ushoga (homosexuality) na msenge (transgender). Pia ukurasa una mawazo mengi ya nafsi kuhusu dini yanayoweza kutofautiana mtu kwa mtu. Hata unarejea mtu kana kwamba angekuwa mtaalamu wa saikolojia, lakini yeye si mwanasaikolojia. Kwa sababu hiyohiyo ya kuwa suala nyeti sana, Wikipedia lazima iwe chanzo kisichopendelea upande wowote. Kisare (majadiliano) 13:08, 7 Aprili 2024 (UTC)
- Tafadhali, soma kwanza jibu langu kwa Kiingereza katika ukurasa wako. Sisi ni wakabidhi wa Wikipedia ya Kiswahili ambao tumekubaliana kuhusu suala hilo. Si kwamba ukurasa hauwezi kuboreshwa, lakini si namna unavyofanya wewe kama kwamba ni mmiliki wa ukweli. Amani kwako! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 13:56, 7 Aprili 2024 (UTC)
Ushirikiano
[hariri chanzo]Ndugu, nakuhimiza tena kupenda ushirikiano na sisi tulioshughulikia Wikipedia hii kwa muda mrefu (mimi miaka 15). Usichukue peke yako maamuzi ambayo unayaona sahihi lakini wengine wanaweza kuona tofauti. Nitoe mfano mmoja mdogo: katika haririo lako la mwisho la ukurasa juu ya Msenge umebadilisha tu neno tanbihi kuwa marejeo. Je, kuna sababu ya kutosha? Umefuta madondoo mengi kwa kudai vyanzo havifai, lakini umeweka vyanzo vingine ambavyo vinatetea hata dawa za kuzuia ubalehe, ukisema hakuna uthibitisho kwamba nchi nyingi zimezikataza. Kwanza sikuandika "nyingi" ila "mbalimbali", lakini hujui kwamba majimbo zaidi ya 10 ya Marekani, Uswidi, Ujerumani na mwezi uliopita hata Uingereza (https://inews.co.uk/news/nhs-england-children-puberty-blockers-2952816?ico=related_stories) zimezikataza kutokana na madhara yake? Pamoja na kufanya mabadiliko mengi, hujaona shida ya msingi ni nyingine, yaani jina la ukurasa: Msenge si tafsiri ya transgender. Kwa jumla ni tusi. Aliyeanzisha makala alilitumia na sisi hatujaona mbadala, ingawa nilishirikisha wenzetu. Ndiyo sababu unakuta katika ukurasa wa ushoga maneno mengine yanahusu transgenders. Ni kama kwamba neno ushoga linabeba makundi yote ya LBGT+, hata kama neno lesbian lina tafsiri yake, msagaji.
Wewe unasisitiza kwamba Wikipedia si mahali pa kutangaza dini na siasa. Kweli kabisa. Lakini kuarifu kuhusu misimamo ya dini si kuzitangaza. Hata kwa Kiingereza ukurasa juu ya Homosexuality unaeleza misimamo hiyo. Sasa, kwa nchi kama hizi za Afrika Mashariki, ambapo dini inatazamwa kuwa muhimu sana katika maisha, iwe Ukristo, Uislamu, Uhindu au nyingine yoyote, taarifa hizo zinatafutwa sana. Inategemea taarifa inavyotolewa, isiwe kama hotuba. Vilevile, kusema mtu anatakiwa kushinda woga ili kuwajibika maishani? Si sharti la saikolojia? Naomba ufikirie hoja hizo ili tujenge pamoja Wikipedia hii. Halafu tuone namna ya kuboresha pamoja hata makala ya Ushoga. Amani kwako! Riccardo Riccioni (majadiliano) 08:44, 10 Aprili 2024 (UTC)
- Umesoma makala hizo unazorejea? Hizo ni nchi ambazo zimeamua kusimamisha dawa za kubadilisha jinsia kwa watoto tu, si watu wote. Makala ya wikipedia kama yalivyoandikwa hayakubainisha hiyo. Hadi kutegeneza kwangu, makala yalisema kwamba dawa "zimesimamishwa" katika nchi mbalimbali. Pia yalizungumza juu ya madhara tu ya dawa hizo, kama kwamba hakuna manufaa yoyote.
- Juu ya hayo, karibu kila chanzo hakikuaminika. Katika sehemu yoyote ya Wikipedia nje ya Wikipedia ya Kiswahili, makala hayo yangalitupwa. Hayafikii viwango vya kimsingi vya Wikipedia (tazama: NPOV, na UCoC) au Wikipedia ya Kiswahili (tazama: Mwongozo).
- Najua maneno yanayomaanisha "gay, transgender, n.k." kwa Kiswahili hayalingani na maneno yanayotumika kwa Kiingereza. Kwa kweli utumiaji "msenge" katika makala ili kumaanisha "transgender" ulinishangaza kwani haimaanishi hivyo. Lakini sikutaka kubadilisha hiyo kwa sababu kutafsiri neno hilo ni suala gumu sana. Jambo muhimu zaidi lilikuwa kutengeneza taarifa kosefu mno.
- Tatizo siyo "kuarifu kuhusu misimamo ya dini". Tatizo ni kueleza misimamo hiyo kama ukweli badala ya msimamo mojawapo kati ya mingi. Tatizo ni kusahau kueleza muktadha muhimu sana. Tatizo ni kufanya madai yasiyothibitishwa na marejeo. Tatizo ni kuandika "kila mmoja anatakiwa...". Wikipedia si mzazi wetu, wala kasisi wetu, wala biblia yetu, wala kurani yetu. Wikipedia ni kamusi.
- Sasa naona kwamba wewe ni mtu aliyeandika sehemu kubwa ya makala hayo kuhusu msenge na taarifa yake kosefu, hivyohivyo kama makala kuhusu "ushoga". Lazima ujifunze kutenganisha maoni yako binafsi ukiandika makala ya Wikipedia kuhusu masuala nyeti. Kisare (majadiliano) 10:58, 10 Aprili 2024 (UTC)
Kukufungia kwa muda
[hariri chanzo]Ndugu Kisare,
Wikipedia yetu ya Kiswahili ina utaratibu wake ikiwemo kushughulikia mijadala mbalimbali inayohusu uboreshaji wa Wikipedia yetu kwa ujumla ikiwemo kupeleka mada inayohitaji mjadala katika ukurasa rasmi wa Jumuiya, kitu ambacho hujafanya na kukimbilia majukwaa ya mbali kabla hujaleta mada husika katika Wikipedia iliyo kiini cha unachokilalamikia. Umeenda mbali zaidi na kusema kwamba Wikipedia ya Kiswahili haina nyenzo za kutatua migogoro na tofauti kama hizi, jambo ambalo si kweli na linaonyesha dharau kwa jumuiya yetu.
Tunatambua na kuheshimu utofauti wako wa kimtazamo kwa baadhi ya makala katika Wikipedia yetu hasa mada za Ushoga/Mapenzi ya jinsia moja, hata hivyo, kulazimisha kubadili kwa kiasi kikubwa kilichokuwepo na kukiweka kadri ya mtazamo wako haikubaliki ili kulinda utofauti na mizania ya makala husika na utofauti wa wachangiaji wenzetu. Iwapo una mawazo ya kuongeza katika makala fulani, ni sawa kuongezea kwa kufuata misingi ya Wikipedia, lakini si sawa kutoa kabisa kiasi kingi cha michango ya wengine na kulazimisha michango yako tu ndiyo ikubalike. Hivyo ili kutunza makala zilizopo kutopata mabadiliko kutoka kwako, nalazimika kukusimamisha kwa muda mpaka pale utakapoacha kupuuzia jumbe za wakabidhi wa Wikipedia yetu na kukubali kufuata taratibu zote za Wikipedia yetu ikiwemo kuheshimu wakabidhi wanaofanya kazi kubwa ya kujenga Wikipedia hii kwa kujitolea kama wewe. Asterlegorch367 (majadiliano) 21:53, 13 Aprili 2024 (UTC)
- Haikuwa nia yangu kuonyesha dharau kwa jumuiya. Kwa kweli nilidhani hakukuwa na nyenzo katika Wikipedia ya Kiswahili kwa kuwa hii ni jumuiya ndogo na taarifa kosefu za makala hayo zilikuwako hapo kwa muda mrefu. Hayo ndiyo kosa yangu.
- Hata hivyo, sidhani ni haki kunifungia kwa kusahihisha makala ambayo yalikiuka kanuni nyingi za Wikipedia na Wikipedia ya Kiswahili, na kwa kupiga ripoti ya ukiukaji huu. Kisare (majadiliano) 22:35, 13 Aprili 2024 (UTC)
- Vipi ninaweza kukata rufaa kuhusu kufungiwa? Kisare (majadiliano) 22:53, 13 Aprili 2024 (UTC)
- Ndugu, kama huta ahidi kujirekebishi na kufuata miongozo unayopewa na jumuiya yetu pamoja na wachangiaji wengine hatutaweza kukuvumilia . amani kwako Hussein m mmbaga (majadiliano) 06:30, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Kujirekebisha kwa nini? kwa kuripoti mchangiaji mwengine aliyekiuka miongozo hiyohiyo? Kisare (majadiliano) 06:35, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Si vyema kuleta tamaduni zako sehemu ambazo hazitakiwi ukikatazwa unapaswa kuacha na kuendelea na mengine yanayokubalika. Ukifanya hivyo utaishi na jumuiya yetu vizuri Hussein m mmbaga (majadiliano) 06:47, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Vipi ninaleta "tamaduni zangu" hapo? Mwongozo wa swwiki na mwongozo wa wikipedia ya jumla ni wazi kabisa; kwa mujibu wa mwongozo huohuo unaorejea, wikipedia si mahali pa "kusambaza maoni kama ukweli... hasa kwenye mada kama dini au siasa." Lakini, hakuna mtajo mmoja kuhusu kwamba kuripoti ukiukaji wa kanuni hizo ni ukiukaji wa kanuni hizohizo. Kisare (majadiliano) 06:59, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Sawa, kwa kweli mmenichosha. Nimechanga kabisa kwenye wikipedia hii, nimeumba jedwali la nchi, jedwali la sayari, nimeandika makala kuhusu HDI, GDP, mjongeo, lenzi za uvutano, Batinilhuti, kisahani cha uongezekaji, viini vya galaksi hai, nyotamwako, nusuranyota, n.k. Nimetafsiri ramani nyingi za nchi kwa Kiswahili. Siku hizi watu wachache wanachanga kiasi hiki. Nafanya haya kwa sababu ya umuhimu wa Kiswahili kama lugha ya Kiafrika, na kwa kuwa ni sehemu ya utamaduni wangu. Swwiki inaweza kuwa chanzo kizuri cha taarifa kisichopendelea upande wowote. Lakini wakabidhi mna maoni mengine. Hawathamani michango yangu, basi nitaacha kuchanga. Nimechoka. Kwa heri na amani kwako. Kisare (majadiliano) 08:11, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Ni kweli ndugu @Kisare Tuna heshimu sana mchango wako kwenye wikipedia ya kiswahili na tunashukuru sana, lakini kufungiwa huku si tu kwa sababu umeenda kusema kwenye majukwa ya mbali, tu bali ni kwasababu bado tunalinda tamaduni zetu za Kiafrika hasa kwenye jumuiya ya Kiswahili. Justine Msechu (majadiliano) 08:33, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Ndugu Kisare, usichoke, kwanza elewa ni nini hasa umekosea, jadili kwa utulivu kufikia muafaka, elewa kua jamii yetu na Wikipedia ya Kiswahili zimefika hapa zilipo si tu kwa juhudi za watu binafsi bali wachangiaji mbalimbali waliokua tayari kushirikiana na kuondoa tofauti zao na kufanya kitu kwa maeleano kama jamii na si ubinafsi. Unakaribushwa kujadili kufikia maelewano na wanajamii wa Wikipedia ya Kiswahili. Czeus25 Masele (majadiliano) 08:51, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Riccardo aliniita mbeberu, na Hussein sasa hivi anasema naleta tamaduni zangu sehemu ambazo hazitakiwi. Sijaingiza maoni yangu yenyewe wala tamaduni zangu kwenye makala yoyote. Hutaona mfano mmoja wa hiyo. Kwa kweli, niliingiza vyanzo pekee katika makala Ushoga vinavyotoka Afrika. Pia niliingiza vyanzo vielezavyo misimamo ya dini kuhusu ushoga, kama vile katekisimu katoliki. Lakini sikuandika kuhusu maoni yoyote kwa upendeleo, kufuata miongozo. Pia niliandika kuhusu maoni ya wanasaikolojia. Hata nilirejea wanasaikolojia wa Afrika Kusini badala ya vyanzo vya magharibi tu. Na kwa michango hiyo nimefungiwa. Kuandika kuhusu saikolojia bila upendeleo ni ubeberu? Haieleweki. Kisare (majadiliano) 10:31, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Si vyema kuleta tamaduni zako sehemu ambazo hazitakiwi ukikatazwa unapaswa kuacha na kuendelea na mengine yanayokubalika. Ukifanya hivyo utaishi na jumuiya yetu vizuri Hussein m mmbaga (majadiliano) 06:47, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Kujirekebisha kwa nini? kwa kuripoti mchangiaji mwengine aliyekiuka miongozo hiyohiyo? Kisare (majadiliano) 06:35, 14 Aprili 2024 (UTC)
- Ndugu, kama huta ahidi kujirekebishi na kufuata miongozo unayopewa na jumuiya yetu pamoja na wachangiaji wengine hatutaweza kukuvumilia . amani kwako Hussein m mmbaga (majadiliano) 06:30, 14 Aprili 2024 (UTC)
Upo huru sasa! Tamba!
[hariri chanzo]Ndugu Kisare,
Upo huru kufanya chochote kile upendacho. Hata ukijisikia kuifunga kabisa Wikipedia ya Kiswahili. Feel free! Hatutakufuata wala kukuhoji kwa chochote kile. Obviously mwenzetu una nguvu sana kuliko sisi. Kila kheri! Muddyb Mwanaharakati Longa 06:23, 20 Mei 2024 (UTC)
Jedwali la nchi
[hariri chanzo]Ukiona upo tayari kushikilia jukumu la kuboresha kabisa utaniambia niondoe zuio lake. Mwanzo ulibadili ukaishia njiani. Hiyo inahesabika kama uharibifu kwa sababu makala zote za nchi zinatumia kigezo hicho. Pia mawasiliano duni yalileta mtafaruku. Kuna umuhimu mkubwa sana wa kujihusisha na majadiliano ya mara kwa mara katika mradi huu. Kwani inaleta undugu na uhusiano mwema. Nje ya hapo watu wanajisikia kudharaulika. Kitu ambacho si kizuri. Inaweza kuwa kwa masukudi au bahati mbaya. Yote kwa yote, karibu sana! Muddyb Mwanaharakati Longa 03:58, 22 Mei 2024 (UTC)
Elimuanga
[hariri chanzo]Ndugu, ulibadili umbo la astronomia kwenda elimuanga. Kipala alikuwa anajua kabisa astronomia ni FALAKI Kwa Kiswahili sanifu cha KAST. Ulipokuja, ukabdili kwenda elimuanga. Je, kuna marejeo yoyote yale ya kitalaamu yanayorejea astronomy kuwa elimuanga? Ninapata ukakasi kidogo. Tazama kamusi ya TUKI inasema hivi; astronomy n falaki. astronomer n Muddyb Mwanaharakati Longa 04:05, 22 Mei 2024 (UTC)
- Hiyo ndiyo niliyofanya muda mrefu uliopita. Wakati ule nilikuwa nimejiunga na jumuia majuzi na kwa kweli nilikuwa mpumbavu kidogo haha.
- Inaonekana kuwa jina la kwanza la makala lilikuwa "falaki" na baada ya muda fulani lilibadiliwa kwenda "astronomia" kufuata ushauri wa mtaalamu wa OUT. Lakini sipendi kutanguliza maneno ya Kiingereza ingawa kuna maneno sanifu ya Kiswahili.
- "Elimuanga" sio sanifu. Hata hivyo, baadhi ya watu wanaitumia. Niliona hapa kwenye kamusi ya TUKI, hapa, na hapa. Lakini ni adimu sana. Kwa sababu hiyo nadhani tutupe "elimuanga".
- Kwa kweli napenda zaidi "falaki". Ina historia katika Kiswahili, na imekubaliwa na TUKI kama ulivyoonyesha. Kiarabu pia hutumia neno falak (chanzo cha neno "falaki").
- Unafikiriaje? Kisare (majadiliano) 06:24, 22 Mei 2024 (UTC)
- Sasa kwa maelezo hayo ya Kipala, kwamba Dkt. Jiwaji aliona kuna unajimu. Unajimu ni kama utabiri wa nyota. Wakati kimsingi astronomia ni zaidi ya falaki ambayo Jiwaji aliona tafsiri ya Kiarabu ni kama utabiri nyota. Lakini pia astronomia si baya ukilitazama kwa umbo la muktadha. Kipala aliunda hadi kamusi ya astronomi. Bahati mbaya, amefariki ikiwa katika umbo ghafi. Mungu amrehemu mzee wetu. Katika kuhitimisha zoezi hili, na kuhshimu juhudi kubwa aliyoiweka Kipala, ninahitimisha tubaki na jina la astronomia. Pia katika mabano tunaongeza, (Pia; Elimuanga au Falaki). Unaonaje? Muddyb Mwanaharakati Longa 07:11, 22 Mei 2024 (UTC)
- Nafurahi kuona mawasiliano yenu. Binafsi nabaki na mtazamo wa Kipala kwamba falaki ni fani ya mnajimu (astrologue), astronomia au elimuanga ni fani ya mwanasayansi (astronome). Amani kwenu! --Riccardo Riccioni (majadiliano) 12:11, 22 Mei 2024 (UTC)
- Hoja hiyo ina maana... Mara nyingi watu wanatumia "falaki" kama "astrology". Pengine falaki si uchaguzi mzuri... Na labda hatuwezi kufuata kabisa TUKI kuhusu jambo hilo, kwa sababu baadhi ya kamusi zake zinatafsiri "unajimu" kama "astronomy"!
- Sipendi "astronomia" kwa sababu ilitokana karibu moja kwa moja na Kiingereza. Pia kuunga kwa konsonati "str" si kawaida katika Kiswahili.
- Sasa nimerudi kupendelea "elimuanga"... Hii ni mifano mingine ya matumizi ya "elimuanga/elimu ya anga": [1][2][3]. Sikulitunga neno. Kisare (majadiliano) 03:15, 24 Mei 2024 (UTC)
Majadiliano katika makala ya Mzunguko
[hariri chanzo]Ndugu Kisare,
Pole kwa kazi nyingi. Nimeweka maoni yangu katika ukurasa wa Mzunguko ambao awali uliitwa njiamzingo. MuddybLonga 10:10, 5 Oktoba 2024 (UTC)
- Nimekujibu! :) Kisare (majadiliano) 02:57, 14 Oktoba 2024 (UTC)