Mjongeo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mjongeo ni uwanja wa fizikia na hisabati ulioendelezwa katika umakanika kawaida, na hueleza mwendo wa nukta, gimba, na mifumo ya magimba bila kuzingatia kani zinazosababisha mwendo wake.[1][2][3][4] Tatizo la mjongeo huanza na kueleza jiometri ya mfumo na kutaja hali ya za viasi vijulikanavyo vya mahali, kasimwelekeo, na mchapuko katika mfumo. Kwa hivyo kutumia kanuni za kijiometri, viasi visivyojulikana vinaweza kutatuliwa, kama vile mwendo wa baadaye wa gimba.

Mjongeo hutumika katika elimuanga ili kueleza mwendo wa violwa vya angani na makundi ya violwa hivyo. Katika uhandisi, mjongeo hutumika ili kueleza mwendo wa sehemu ziunganazo za mashine kama vile injini.

Asili ya neno[hariri | hariri chanzo]

Katika Kiswahili, jina la elimu hii ni "mjongeo", kutokana na kitenzi "jongea". Istilahi hii iliundwa na wataalamu wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili.[1] Katika lugha za Kizungu, jina hutokana na istilahi ya Kifaransa cinématique, kama ilivyoundwa na A.M. Ampère,[5] ambayo yenyewe ilitokana na Kigiriki κίνημα kinema (yaani "mwendo"). Kwa hiyo, lugha za Kizungu hutumia istilahi inayofanana na ile ya Kifaransa, kama vile kinematics (Kiingereza), cinemática (Kihispania), kinematik (Kijerumani), na kadhalika.

Milinganyo ya mjongeo[hariri | hariri chanzo]

Taswira 1: Jiometri ya mjongeo

Taswira 1 kijiometri inaonyesha jinsi ilivyonyambua milinganyo ya msingi wa mjongeo. Kwenye jira wima kuna kasi (), na kwenye jira mlalo kuna muda (). Yaani taswira inaonyesha kadiri ambayo kasi inabadilika wakati ukipita; uhusuiano huu ni mstari mwenye mwinamo, unaoonyesha kasi inaongezeka. Mwinamo wa mstari huu ni mchapuko (). Kijiometri, hiyo inamaanisha eneo kati ya mstari na jira ya muda (eneo jekundu katika taswira) ni umbali uliosafiriwa katika muda huohuo, kwa sababu kizio cha jira ya kasi ni mita kwa sekunde () na kile cha jira ya muda ni sekunde (). Hivyo, kizio cha eneo ni , yaani tu, iliyo kizio cha umbali.

Toka huko, umbali uliosafiriwa katika muda na kwa kasi ya kwanza unatambulishwa:

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 Kamusi Sanifu ya Biolojia, Fizikia na Kemia. Chuo Kikuu cha Dar es Salaam: TUKI. 1990. uk. 101. ISBN 9976911092.
  2. Edmund Taylor Whittaker (1904). A Treatise on the Analytical Dynamics of Particles and Rigid Bodies. Cambridge University Press. Sura 1. ISBN 0-521-35883-3.
  3. Joseph Stiles Beggs (1983). Kinematics. Taylor & Francis. uk. 1. ISBN 0-89116-355-7.
  4. Thomas Wallace Wright (1896). Elements of Mechanics Including Kinematics, Kinetics and Statics. E and FN Spon. Sura 1.
  5. Ampère, André-Marie (1834). Essai sur la Philosophie des Sciences. Chez Bachelier.
Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mjongeo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.