Mchapuko

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Mchapuko (pia mchapuo, kwa Kiingereza acceleration) ni istilahi ya fizikia inayotaja badiliko la kasi au zaidi kasimwelekeo ya kitu kwa kipindi fulani. Mchapuko unafafanuliwa kuwa badiliko la kasimwelekeo (velositi) linalogawiwa kwa badiliko la wakati.

Mchapuko unatokea kama gimba linaongeza kasi, linapunguza kasi au linabadilisha mwelekeo wake. Mfano gari linalopiga mbio, linalopigwa breki au kupiga kona linaona mchapuko.

  • Kama gari lililosimama linaanza kutembea mbele linaingia katika mchapuko kimstari (ing. linear acceleration) na abiria ndani yake wanaisikia kama kani inayowasukuma nyuma dhidi ya viti vyao.
  • Wakati gari linapita kona ya barabara linaingia katika mchapuo usio kimstari (non-linear acceleration) na abiria wanaweza kusikia kani inayowasukuma kwa upande wa nje.
  • Kama dereva anapiga breki gari linaingia katika mchapuo hasi (deceleration) yaani mchapuko kinyume cha mwendo wake hadi sasa na hapo abiria husikia kani inayowasukuma mbele.

Kipimo cha SI cha mchapuko ni m/s2 yaani mraba wa mita kwa sekunde.

Makala hii kuhusu mambo ya fizikia bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mchapuko kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.