Kasimwelekeo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Kasimwelekeo, pia velositi[1] (ing. velocity) ni kipimo cha kutaja kasi ya mwendo wa kitu kuelekea mahali fulani. [2]

Katika fizikia kasimwelekeo inataja muda unahitajika kupeleka kitu kutoka mahali pamoja kwenda mahali pengine. Kwa hiyo ni kipimo kinachounganisha habari mbili yaani kasi na mweleko. Kipimo cha aina hii huitwa kipimo vekta.

Kwa mfano gari inaelekea kusini kwa kasi ya 70 km/h. Habari hizi kwa pamoja ni kasimwelekeo. [3]

+ mwelekeo.[2]

Kama kitu kinazunguka kwenye duara mara moja na kufikia pale kilipotoka hakikuondoshwa. Kwa hiyo uondoshaji wake ni = sifuri na hivyo hata kasimwelekeo ni sifuri. Hii ni tofauti na kasi ya kitu kile katika mwendo wa kuzunguka.

Kasimweleko ni lazima kuwa na mwelekeo pia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Kamusi ya TUKI KKK/ESD inataja "kasimwelekeo", TUKI-KAST inataja "velositi"
  2. 2.0 2.1 Physics Homework Help: Speed, Velocity, Acceleration. physics247.com. Iliwekwa mnamo 25 March 2010.
  3. Vectors, Introduction. id.mind.net. Iliwekwa mnamo 25 March 2010.

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: