Km/h

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mita hii katika gari ni tayari kuonyesha kasi kwa km/h

Km/h (kifupi cha "Kilomita kwa saa") ni kipimo cha kasi. Km peke yake ni kifupi cha kilomita na h ni kifupi cha saa (kutoka Kilatini hora > Kiingereza hour).

Kitu chenye kasi ya km/h 1 (kilomita moja kwa saa) kinatembea kilomita moja katika muda wa saa moja. Mwanadamu kwa mwendo wa wastani anatembea kwa km/h 5 yaani katika muda wa saa moja anatembea kilomita tano. Kwa kutumia baisikeli kwa kasi ya wastani mtu husafiri kwa km/h 15 hadi km/h 20. Magari yanaruhusiwa kusafiri kwa 50 km/h mijini na 80 hadi km/h 100 nje ya miji.

Kipimo cha SI kwa kasi ni m/s yaani mita kwa sekunde lakini hakitumiki sana kwa sababu katika maisha ya kila siku watu hawataki kujua mwendo wao kwa kila sekunde.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Km/h kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.