Kiini cha majarra hai

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Centaurus A ni mfano wa majarra hai.

Kiini cha majarra hai (kwa kiingereza: active galactic nucleus) ni eneo dogo lenye maada nyingi kwa karibu katika kitovu cha majarra ambayo inayonururisha nishati pote pa taswirangi sumakuumeme. Huwa na sifa bainifu zinazoonyesha kuwa mng'aro wake hutolewi na nyota. Utokezaji mno kama huu usiotokana na nyota umechunguzwa kwa mawimbiredio, mawimbimikro, mialekundu, nuru inayoonekana, urujuanimno, miali-X, na miali gama. Majarra yenye kiini hai ni majarra hai. Imetolewa nadharia kuwa mnururusho usiotokana na nyota husababishwa na uongezekaji wa maada kwa shimo jeusi la tungamomno kwenye kitovu cha majarra yake yenyeji.

Viini vya majarra hai ni vyanzo angavu kuliko vyote vya mnururisho sumamkuumeme ulimwenguni na kwa hivyo vinaweza kutumiwa kama mbinu wa kugundua violwa vya mbali. Pia, mageuko yake yategemeayo wakati wa ulimwengu yanazuia maelezo ya kisayansi ya ulimwengu.

Vijamii vingi vya viini hai vimeainishwa kwenye msingi wa sifa bainfu zake ambazo zimeangaliwa; Viini hai vyenye nguvu zaidi huainishwa kama nusuranyota. Nyotamwako ni kiini hai chenye mchirizi ambao umeelekea duniani, na mnururisho wa mchirizi huongezwa na kuangaza husianifu

Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kiini cha majarra hai kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.