Lupita Nyong'o

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Lupita Nyongo(2013)
Lupita Nyongo (2016)

Lupita Nyong’o (alizaliwa 1 Machi 1983) ni mwigizaji kutoka Kenya na Meksiko. Mwenyewe anajitambulisha kutoka nchi hizo mbili, kwa sababu ana uraia wa nchi hizo.

Maisha[hariri | hariri chanzo]

Yeye ni mtoto wa mwanasiasa nchini Kenya Peter Anyang' Nyong'o na Dorothy Ogada Buyu. Lupita alizaliwa mji wa Mexiko, katika nchi ya Mexiko, kwa sababu baba yake alifundisha sayansi ya siasa katika chuo ya Mexiko, katika Mji wa Mexiko. Familia yake waliondoka nchi ya Kenya katika mwaka wa 1980 kwa muda mfupi kwa sababu kulikuwa na matatizo kuhusu siasa na baba yake hakutaka kukaa huko. Ndugu wa baba yake Lupita, Charles Nyong’o, alirushwa nje ya feri na kupotea[onesha uthibitisho].

Lupita ni Mluo, kwa sababu baba na mama yake wanasema lugha ya Kijaluo. Katika kabila la Wajaluo, Waluo wanapenda kupatia majina kwa watoto wao kulingana na matukio ya siku, hivyo, walimpatia jina la Lupita[onesha uthibitisho].

Familia ya Lupita walirudi nchini Kenya wakati Lupita alipokuwa na umri wa mwaka mmoja, kwa sababu baba yake alipata kazi katika Chuo Kikuu cha Nairobi. Lupita alikulia katika mji wa Nairobi[onesha uthibitisho].

Akiwa na umri wa miaka kumi na nne, Lupita alianza ukumbi wa michezo kwa kucheza Juliet katika tamthilia Romeo na Juliet, kwa kampuni ya Phoenix Players. Wakati Lupita akifanya kazi katika kampuni hiyo, alicheza michezo ya On the Razzle, na There Goes The Bride. Lupita alitaka kufanya kwenye ukumbi wa michezo kwa sababu alipenda Whoopi Goldberg na Oprah Winfrey[onesha uthibitisho].

Wakati Lupita alipokuwa na umri wa miaka kumi na sita, wazazi wa Lupita walimtuma kwenda nchi ya Mexiko kusoma lugha ya Kihispania kwa miezi saba. Lupita aliishi jiji la Taxco, jimbo la Guerrero, na alisoma katika chuo kikuu cha Mexiko[onesha uthibitisho].

Lupita alisoma masomo za filamu na masomo za ukumbi wa michezo katika chuo cha Hampshire[onesha uthibitisho].

Lupita alianza kazi yake ya msaidizi wa uzalishaji katika jiji la Hollywood. Katika mwaka wa 2008, alianza kutenda na filamu ndogo yake ya kwanza, East River. Alirudi nchi ya Kenya kutenda kwa tamthiliya Shuga (2009-2012). Katika mwaka wa 2009 pia Lupita aliandika na alielekeza maandishi In My Genes. Baadaye, alikwenda kusoma kaimu katika Chuo Kikuu cha Yale. Baada ya kupata shahada ya pili, alikutenda kama Patsey, katika mchezo wa 12 Years a Slave. Alishinda tuzo nyingi, ikiwamo tuzo wa mwigizaji bora. Yeye alikuwa Mkenya na Mmexiko wa kwanza kushinda tuzo ya taasisi[onesha uthibitisho].

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mwigizaji filamu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Lupita Nyong'o kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.