Nenda kwa yaliyomo

Sulwe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Sulwe ni jina la kitabu cha watoto ambacho kiliandikwa na mwigizaji na mshindi wa tuzo ya Academy[1] anayeitwa Lupita Nyong’o.[2][3] Vashti Harrison ni mchoraji wa kitabu hicho.[4]

Muhtasari

[hariri | hariri chanzo]

Kisa hiki kinamfuata msichana ambaye anaitwa Sulwe. Sulwe ana wasiwasi kutokana na rangi ya ngozi yake. Rangi ya ngozi yake ni nyeusi zaidi kuliko wanafamilia wao na wanafunzi wenzake. Sulwe anataka rangi ya ngozi yake isiwe nyeusi. Kwa hivyo, yeye anajaribu kutafuta njia ya kubadilisha rangi ya ngozi yake nyeupe. Kwa hivyo, Sulwe anaanza safari ya kichawi ambayo inabadilisha kila kitu. Katika safari hiyo, Sulwe anajifunza kwamba umuhimu, urembo, na uzuri wa mtu hauhusiani wala hautegemeani na rangi ya ngozi ya mtu. Hatimaye, anajifunza kupenda rangi ya ngozi yake na wasiwasi wake unakoma.

Uhamasishaji

[hariri | hariri chanzo]

Wakati Lupita Nyong'o alipokuwa mtoto, yeye alikuwa na wasiwasi kutokana na rangi ya ngozi yake, sawa na Sulwe.[5] Yeye anakumbuka kwamba alikuwa akijitambua katika shule yake, na aliogopa mtazamo wa wanafunzi wenzake juu ya rangi ya ngozi yake. Kama Sulwe, Bi Nyong’o alifikiri kwamba rangi ya ngozi ya aina ya dada yake, ambaye ana rangi ya ngozi yenye kung’aa, ilionekana kuwa “nzuri”. “Kwa kweli, nilikuwa sijisikii vizuri na rangi yangu ya ngozi kwa sababu nilihisi kuwa ulimwengu ambao ulikuwa ukinizunguka uliwapa watu tuzo kwa rangi za ngozi zenye kung’aa zaidi.”[6]

Mwaka wa 2019, Bi Nyong’o alialikwa katika mahojiano na NPR ili kuzungumza juu ya kitabu chake. Katika mahojiano hayo, alikubali kwamba, kama Sulwe, alipokuwa na umri wa miaka mitano tu, alimuomba Mungu kubadilisha rangi ya ngozi yake iwe nyeupe kwa sababu hakutaka rangi ya ngozi yake iwe nyeusi.[7] Pia, wakati alipokuwa katika darasa la pili katika shule ya msingi, mwalimu wake alimwambia kwamba yeye hataolewa kwa sababu ya ngozi yake nyeusi.

"Watu hawatambui wanachofanya wanaposema maneno ya aina hii… Wao wanafikiri kusema vitu vya aina hii si mbaya. Lakini kweli wanachofanya ni hatari sana na msichana mdogo katika ulimwengu ambamo kuna ukumbusho chache sana kwamba yeye ni muhimu kwa jinsi alivyo."[7]

Zaidi ya habari hiyo, kabla ya kuwa na mmoja wa waigizaji maarufu katika dunia, Bi Nyong’o aliambiwa katika mahojiano kwamba yeye hawezi kuwa mwigizaji kwa sababu ya rangi ya ngozi yake.[8][9]

Tuzo kwa Sulwe

[hariri | hariri chanzo]

Muuzaji Bora wa New York Times[10]

Coretta Scott King Tuzo ya Mchoraji Wa Heshima[11][12]

Mshindi, Kazi ya Fasihi Inayojitokeza - Watoto 51 NAACP Image Awards 2020[13]

  1. "2014 | Oscars.org | Academy of Motion Picture Arts and Sciences". www.oscars.org (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-03-31.
  2. Gyarkye, Lovia (2018-01-17), "Lupita Nyong'o to Publish a Children's Book", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2023-03-31
  3. "SULWE by Lupita Nyong'o and Vashti Harrison". sulwebylupita.com (kwa American English). Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2023-02-25. Iliwekwa mnamo 2023-03-31.
  4. Russo, Maria (2019-10-14), "Vashti Harrison Lets the Light In", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2023-03-31
  5. Good Morning America. "Lupita Nyong'o pens children's book starring a child learning to love her dark skin". Good Morning America (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-03-31.
  6. "Lupita Nyong'o kuchapisha kitabu cha watoto", BBC News Swahili, iliwekwa mnamo 2023-03-31
  7. 7.0 7.1 NPR. (2019, October 17). Lupita Nyong'o on 'Sulwe'. NPR. Retrieved March 31, 2023.
  8. Condé Nast (2016-09-16). "Lupita Nyong'o Claps Back at People Who Said Her Skin Color Would Hurt Her Success". Glamour (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-03-31.
  9. Condé Nast (2016-09-15). "Lupita Nyong'o: "I Want to Create Opportunities for People of Color"". Vogue (kwa American English). Iliwekwa mnamo 2023-03-31.
  10. "Children's Picture Books - Best Sellers - Books - Nov. 10, 2019 - The New York Times", The New York Times (kwa American English), ISSN 0362-4331, iliwekwa mnamo 2023-03-31
  11. "Sulwe | Awards & Grants". www.ala.org. Iliwekwa mnamo 2023-03-31.
  12. American Library Association (2012-04-05). "Coretta Scott King Book Awards - All Recipients, 1970-Present". Round Tables (kwa Kiingereza). Iliwekwa mnamo 2023-03-31.
  13. "The Nominees | NAACP Image Awards". web.archive.org. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2020-02-28. Iliwekwa mnamo 2023-03-31.
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Sulwe kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.