Whoopi Goldberg

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search
Whoopi Goldberg
Whoopi Goldberg at a NYC No on Proposition 8 Rally.jpg
Goldberg in New York City, Novemba 2008
Amezaliwa Caryn Elaine Johnson
13 Novemba 1955 (1955-11-13) (umri 62)
New York City, New York, US
Kazi yake Mwigizaji, mchekeshaji, DJ wa redio, mtunzi wa vitabu, mwimbaji-mtunzi, mtangazaji wa kipindi cha majadiliano, mwanaharakati
Miaka ya kazi 1981–mpaka sasa
Ndoa Alvin Martin (1973–1979)
David Claessen (1986–1988)
Lyle Trachtenberg (1994–1995)

Whoopi Goldberg (amezaliwa na jina la Caryn Elaine Johnson; mnamo 13 Novemba 1955)[1] ni mchekeshaji, mwigizaji, mwimbaji, mtunzi wa nyimbo, mwanaharakati wa kisiasa, na mtangazaji wa kipindi cha majadiliano kutoka nchini Marekani.

Goldberg ameanza kuonekana katika ulimwengu huu wa filamu kwa mara ya kwanza kwenye The Color Purple (1985) akicheza kama Celie, mwanamke anaye-nyanyasika mjini kusini. Amepokea uteuzi wa Academy Award kwa Mwigizaji Bora na kushinda kwa mara ya kwanza Golden Globe Award kwa uhusika wake katika filamu hiyo. Mnamo 1990, amecheza kama Oda Mae Brown, bingwa wa maono anayemsadia mtu aliyeuawa (Patrick Swayze) kumtafuta mwuaji wake katika filamu bab-kubwa ya Ghost. Kazi hii imempelekea ashinde tuzo ya pili ya Golden Globe na [[Academy Award akiwa kama Mwigizaji Msaidizi. Baadaye akaja-kupata umaarufu zaidi katika mfululizo wa filamu za Sister Act na Sister Act 2, "The Lion King", Made in America, How Stella Got Her Groove Back, Girl, Interrupted na Rat Race . Pia amevuma sana na uhusika wake wa kucheza kama mwuza baa Guinan katika Star Trek: The Next Generation.

Goldberg ameteuliwa mara 13 na tuzo za Emmy Awards kwa ajili kazi zake katika televisheni. Alikuwa mtayarishaji-mwenzi katika kipindi maarufu cha Hollywood Squares kuanzia 1998-2004. Tangu 2007, amekuwa msimamizi wa kipindi cha majadiliano cha TV, The View. Goldberg ana Grammy, Emmy saba, Golden Globes mbili, Tony, na Oscar. Kwa upande mwingine, Whoopi ana British Academy Film Award, People's Choice Awards nne na amepewa heshima yake katika ya nyota katika Hollywood Walk of Fame.

Filmografia[hariri | hariri chanzo]

Filamu[hariri | hariri chanzo]

Television[hariri | hariri chanzo]

Diskografia[hariri | hariri chanzo]

Bibliografia[hariri | hariri chanzo]

  • Goldberg, Whoopi (2006). Whoopi's Big Book of Manners. New York: Hyperion Books for Children. ISBN 078685295X. 
  • Goldberg, Whoopi (1997). Book. New York: R. Weisbach Books. ISBN 068815252X. 
  • Goldberg, Whoopi (1992). Alice. New York: Bantam Books. ISBN 0553089900. 

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Some sources quote her birth year as 1949 and 1950 Biography.comIMDB

Soma zaidi[hariri | hariri chanzo]

  • Adams, Mary Agnes (1993). Whoopi Goldberg: From Street to Stardom. New York: Dillon Press. ISBN 0875185622. 
  • Caper, William (1999). Whoopi Goldberg: Comedian and Movie Star. Springfield, NJ: Enslow Publishers. ISBN 0766012050. 
  • DeBoer, Judy (1999). Whoopi Goldberg. Mankato, MN: The Creative Company. ISBN 0886826969. 
  • Gaines, Ann (1999). Whoopi Goldberg. Philadelphia: Chelsea House. ISBN 0791049388. 
  • Parish, James Robert (1997). Whoopi Goldberg: Her Journey from Poverty to Megastardom. Secaucus, NJ: Carol Publishing Group. ISBN 1559724315. 

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote-logo.svg
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Commons-logo.svg
Wikimedia Commons ina media kuhusu: