Ludoviko IX

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Louis IX alivyochorwa na El Greco 15921595 hivi.
Sanamu ya Mt. Ludoviko IX huko Paris, Ufaransa.
Masalia yake yanatunzwa katika sanduku hili la mwisho wa karne ya 13 katika Basilika la Mt. Dominiko, Bologna, Italia.
Sanamu yake kama mwanajeshi katika Basilika la Moyo Mtakatifu, Paris.

Ludoviko IX (Poissy, karibu na Paris, Ufaransa, 25 Aprili 1214Tunis, Tunisia, 25 Agosti 1270), maarufu kama Mtakatifu Alois, alikuwa mfalme wa Ufaransa tangu 1226 hadi kifo chake.

Anahesabiwa kuwa mtawala bora wa Kikristo kwa jinsi alivyojalia ibada, alivyoheshimu ndoa yake, alivyohudumia wananchi, hasa maskini na wagonjwa, na alivyotetea Wakristo waliodhulumiwa.

Alifariki dunia kwa tauni aliyoambukizwa kwa kuwahudumia askari zake wakati wa vita vya msalaba.

Ni mfalme pekee wa nchi hiyo kutangazwa mtakatifu (na Papa Boniface VIII, 1297).

Sikukuu yake huadhimishwa tarehe aliyoaga dunia[1].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • Davis, Jennifer R. "The Problem of King Louis IX of France: Biography, Sanctity, and Kingship," Journal of Interdisciplinary History Autumn 2010, Vol. 41, No. 2: 209–225. review of Gaposchkin (2008) and Le Goff (2009)
  • Gaposchkin, M. Cecilia. The Making of Saint Louis: Kingship, Sanctity, and Crusade in the Later Middle Ages (Cornell University Press, 2008) 352 pp.
  • Jordan, William Chester. Louis IX and the Challenge of the Crusade: A Study in Rulership (Princeton, 1979), a highly influential study says Davis (2010)
  • Le Goff, Jacques. Saint Louis (University of Notre Dame Press, 2009) 952 pp.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.