Kipanya manyoya-magumu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Lophuromys)
Kipanya manyoya-magumu
Kipanya manyoya-magumu tumbo-kutu (Lophuromys kapusi)
Kipanya manyoya-magumu tumbo-kutu (Lophuromys kapusi)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Deomyinae (Wanyama wanaofanana na vipanya-miiba)
Jenasi: Lophuromys
Peters, 1874
Ngazi za chini

Spishi 21:

Vipanya manyoya-magumu ni wanyama wagugunaji wa jenasi Lophuromys katika nusufamilia Deomyinae ya familia Muridae. Manyoya yao ni magumu lakini siyo kama yale ya vipanya-miiba. Wanatokea katika Afrika kusini kwa Sahara tu, mara nyingi milimani.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Vipanya hao wamepata jina lao kwa sababu wana manyoya magumu. Yanafanana na nywele za brashi nyororo lakini hayafanani na [[mwiba}miiba]] kama manyoya ya vipanya-miiba. Mwonekano wao si wa kawaida kwa sababu kadhaa. Rangi ya manyoya inatofautiana kulingana na spishi; inaweza kuwa hudhurungi au kijivukijani hadi kahawia iliyoiva. Spishi fulani huwa na mng'ao zambarau na nyingine zina madoa. Upande wa chini ni rangi ya kutu, ya machungwa, ya kahawa au ya maziwa.

Hawa ni vipanya wanene wenye miguu mifupi kiasi. Urefu wa mwili ni kati ya sm 8 na 17.5 na wa mkia sm 6-10.

Wengi sana wa wanyama hawa wana makovu, masikio yenye mikato au/na mkia unaokosa sehemu. Ngozi yao ni nyembamba na wanaonekana kutumia hii kama maarifa ya kuzuia mbuai. Mkia huvunjika kwa urahisi kusudi mnyama achopoke. Ukiwa umepoteza haukui tena. Ngozi hupasuka kwa urahisi, haswa katika sehemu zifaazo kama vile kisogo. Kwa ukweli, ikiwa mnyama ameshikwa kwa kisogo, anaweza kujikomboa kwa njia ya kujikonyoa akiacha kiraka cha ngozi pamoja na manyoya. Mifano inayopatikana kwenye makumbusho inaonekana nadra ikikosa mipasuko yaliyoshonwa.

Vipanya manyoya-magumu huishi peke yao na wameripotiwa kupigana wakiwekwa pamoja. Hii inaweza kuchangia vidonda vinavyoonwa kwenye wanyama hao.

Imeandikwa kwamba kipanya manyoya-magumu mmoja ameishi kwa muda wa miaka 3 kifungoni.

Makazi na chakula[hariri | hariri chanzo]

Vipanya manyoya-magumu huonekana kuhitaji maeneo manyevu na labda nyasi. Kwa kawaida hawapatikani katika savana kavu na misitu yenye mfuniko mzito wa majani. Hukiakia mchana au usiku au hata alasiri na alfajiri kulingana na spishi.

Chakula chao kina maada nyingi za wanyama kuliko takriban panya wote. Uwiano wa maada za wanyama katika mlo wao ni 40-100% kulingana na spishi. Huu unajumuisha sisimizi, wadudu na invertebrata wengine, vertebrata wadogo, mizoga na maada za mimea.

Spishi[hariri | hariri chanzo]