Kipanya-miiba
Kipanya-miiba | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kipanya-miiba wa Rasi (Acomys subspinosus)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 21:
|
Vipanya-miiba ni wanyama wagugunaji wa jenasi Acomys katika nusufamilia Deomyinae ya familia Muridae walio na manyoya magumu kama miiba. Wanatokea katika Afrika na Mashariki ya Kati kwenye majangwa na maeneo mengine makavu, pengine misitu mikavu na mara nyingi maeneo yenye mawe na miamba.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Vipanya-miiba hufanana sana na vipanya wa kawaida wa jenasi Mus, lakini hutofautiana kwa kuwa na manyoya magumu sana, kama miiba, na mkia mfupi zaidi ambao wanaweza kumwaga ili kuchopoka. Wana urefu wa sm 8-17.5 na mkia wa sm 4-12 na uzani wa g 18-90, yote kulingana na spishi. Kwa kawaida manyoya huwa kahawia au kijivu au yenye rangi ya nyekundu/machungwa kidogo, mara chache nyeupe au nyeusi; upande wa chini ni mweupe. Huwa na masikio makubwa na pua iliyoelekezwa zaidi kuliko vipanya wa kawaida.
Chakula
[hariri | hariri chanzo]Vipanya hao hula mbegu, maua, mimea ya jangwani, konokono, wadudu na mizoga, lakini spishi kadhaa hula wadudu hasa. Kwa kawaida hawakunywi na hupata maji kutoka kwa chakula chao. Wanatoa mkojo uliokolea ili kuzuia upoteaji wa maji.
Makazi
[hariri | hariri chanzo]Makazi ya vipanya-miiba ni maeneo makavu, kama majangwa, savana na vichaka na misitu mikavu, mara nyingi yenye miamba. Hukiakia usiku au alasiri na alfajiri sana. Spishi kadhaa zinaweza kukiakia mchana. Kwa asilia huishi miaka mitatu kwa wastani, lakini kifungoni wanaweza kuishi zaida ya miaka mitano.
Uzazi
[hariri | hariri chanzo]Kipindi cha ujauzito ni wiki 3-5. Majike huzaa wachanga 2-5 ambao wana manyoya mafupi tayari na macho yaliyofunguka. Majike wanaweza kupandana tena mara tu baada ya kuzaa.
Spishi za Afrika
[hariri | hariri chanzo]- Acomys airensis, Kipanya-miiba wa Sahara Magharibi
- Acomys cahirinus, Kipanya-miiba Kaskazi
- Acomys chudeaui, Kipanya-miiba wa Chudeau
- Acomys cineraceus, Kipanya-miiba Kijivu (Kenya, Uganda)
- Acomys ignitus, Kipanya-miiba Mchomaji (Kenya, Tanzania)
- Acomys johannis, Kipanya-miiba wa Johan
- Acomys kempi, Kipanya-miiba wa Kemp (Kenya, Tanzania)
- Acomys louisae, Kipanya-miiba wa Louise (Kenya)
- Acomys mullah, Kipanya-miiba Mullah
- Acomys muzei, Kipanya-miiba wa Muze (Tanzania)
- Acomys ngurui, Kipanya-miiba wa Nguru (Tanzania)
- Acomys percivali, Kipanya-miiba wa Percival (Kenya, Uganda)
- Acomys seurati, Kipanya-miiba wa Tibesti
- Acomys spinosissimus, Kipanya-miiba Kusi
- Acomys subspinosus, Kipanya-miiba wa Rasi
- Acomys wilsoni, Kipanya-miiba wa Wilson (Kenya, Tanzania, Uganda)
Spishi za Asia
[hariri | hariri chanzo]- Acomys cilicicus
- Acomys dimidiatus
- Acomys minous
- Acomys nesiotes
- Acomys russatus
Picha
[hariri | hariri chanzo]-
Kipanya-miiba kaskazi
-
Kipanya-miiba wa Tibesti
-
Golden spiny mouse
-
Asia Minor spiny mouse
-
Arabian spiny mouse