G

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

G ni herufi ya 7 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni katika alfabeti ya Kilatini.

Maana za G[hariri | hariri chanzo]

Historia ya alama G[hariri | hariri chanzo]

Alama ya G ilianzishwa katika alfabeti ya Kilatini kama badiliko la herufi C.

Kiebrania
gimel
Kifinisia
gimel
Kigiriki
Gamma
Kiitalia
cha awali: C
Kilatini
C (=g / k)
ג Phoenician gimel Classical Greek Gamma Early Latin Late Latin C

Asili ya herufi G ni pamoja na C katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na gimel iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya ngamia wakitumia alama tu kwa sauti ya "g" na kuiita kwa neno lao kwa ngamia "gimel". Wagiriki walichukua alama hiyo na kuiita "gamma" bila kujali maana asilia ya "ngamia" ilikuwa sauti tu ya "g".

Waitalia ya kwanza hawakuwa na sauti ya "g" wakatumia alama kwa aina ya "k". Waroma wakaipokea hivyo lakini walikuwa na sauti ya "g" hivyo mwanzoni walitumia "C" kwa sauti zote mbili za "G" na "K". Baadaye waliona vema kutofautisha kati ya sauti za "k" na "g" wakaongeza mstari kwenye C kuifanya G. "C" ikabaki kwao kwa kuandika sauti ya "k".