Waetruski

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Sanamu ya baba na mama wa nyumba Waetruski (makumbusho ya Firenze)
Mpiga muziki kutoka kaburi la Kietruski

Waetruski walikuwa taifa katika Italia ya kale walioishi katika Italia ya Kati kwenye mazingira ya mji wa Roma. Mwanzo wa ustaarabu wao ulikuwa mnamo mw. 800 KK ukaishia katika miaka ya mwisho wa Jamhuri ya Roma.

Waliacha mabaki ya utamaduni mwenye mifano bora ya uchoraji na ujenzi. Utamaduni wao ulipotea katika mazingira ya Kiroma.

Lugha[hariri | hariri chanzo]

Lugha ya Kietruski haikuwa kati ya lugha za Kihindi-kiulaya. Wataalamu wengi huamini kuwa walihamia Italia kutoka Anatolia. Mwandiko wao uliotunzwa ukutani wa makaburi wasomeka kirahisi kwa sababu ulifuata alfabeti ya Kigiriki pamoja na athira ya Wafinisia wa Mediteranea ya magharibi. Lakini si rahisi kuelewa lugha kwa sababu msamiati ni wa pekee; hadi sasa ni takriban maneno 200 yanayoeleweka.

Waetruski walianzisha miji 12 walioshirikiana kama shirikisho. Inaaminika ya kwamba misingi ya mji wa Roma ni ya Kietruski pia. Wafalme wa Roma walikuwa wa asili ya Kietruski. Hivyo hadi mwaka 396 Roma ilikuwa chini ya athiri ya Waetruski. Mwaka ule jeshi la Roma likateka na kuangamiza mji wa Veiji na kumaliza kipaumbele ya Waetruski katika Italia. Miji kadhaa ya Kietrsuki ilifanya mikataba ya Roma ikapewa uraia wa Kiroma hadi mwaka 90 KK. Baadaye utamaduni wa Kietruski ulianza kupotea wakati watu walipoacha kutumia lugha yao.