Nenda kwa yaliyomo

H

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

H ni herufi ya 8 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Eta ya alfabeti ya Kigiriki.

Maana za H[hariri | hariri chanzo]

Historia ya H[hariri | hariri chanzo]

Kisemiti asilia
ħ
Kietruski
H
Kigiriki
(H)eta
Kifinisia
ħ
Kilatini
H

Asili ya alama ni picha andishi iliyoonyesha fensi. Wafinisia walirahisicha alama na kuitumia kama "khet" yaani h kali yenye matamshi ndani ya shingo. Wagiriki walipokea alama kwa jina "heta" na kuitamka awali kama "h". Katika maendeleo ya lugha waliacha kutamka sauti ya "h" mwanzoni ikabaki sauti ya "e" pekee na alama ikaitwa "Eta" ikiwa na matamshi kama "e" ndefu.

Waetruski walipokea alama kwa umbo la Kifinisia lakini kwa sauti ya "h". Waroma wakaiingiza katika alfabeti ya Kilatini kwa maana ileile yaani kama sauti ya "h" lakini walipendelea umbo la Kigiriki. Hivyo alama yetu ya "H" imepatikana na kubaki hivyo.