Nenda kwa yaliyomo

W

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
Aa Bb Cc Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz
(Kwa matumizi ya Kiswahili)
ch dh gh kh
mb mv nd ng ng' nj
ny nz sh th

W ni herufi ya 23 katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni ipsilon katika alfabeti ya Kigiriki.

Maana za W

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya alama W

[hariri | hariri chanzo]

Historia ya W ina asili za pamoja na U, V, Y na F. Historia hii ni ngumu kidogo kwa sababu alama ilipita katika alfabeti za lugha ambazo zilitumia hasa alama hii kwa sauti tofautitofauti. Kwa sababu hii matamshi yalibadilika kati ya lugha na lugha. Pia lugha mpya iliweza kuona haja ya kuunda alama mpya kwa sauti ya pekee.

Lateinisches W
Kisemiti asilia:
picha ya kingoe
Kifinisia:
Waw
Kigiriki:
ipsilon
Kietruski:
V
Kilatini:
V
Kilatini Kipya:
W

Alama ya W kiasili haikupatikana katika Kilatini cha Kale. Waroma hawakutamka "w" tofauti na "v". Matumizi yake ilikubaliwa wakati wa Kilatini Kipya katika karne ya 16. Wakati ule Kilatini lilikuwa lugha ya kitaalamu ya mataifa ya Ulaya penye wasemaji wengi wa lugha za Kigermanik zilizokuwa na sauti hii lakini iliandikwa kwa kutumia V. Wakati ule wataalamu wa Ulaya walikubaliana kutumia alama ya V mara mbili kwa kuonyesha sauti ile ya w.

Kwa hiyo historia yake ni sawa na V: Waroma walipokea alama hii kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na "waw" iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya fimbo la kingoe au kiopoo. Wagiriki wa Kale walichukua alama hiyo na kuitumia kwa namna mbili: kwa umbo moja kama digamma (tazama F) na umbo la pili kama "ipsilon" bila kujali maana asilia ilitaja sauti kati ya "u" na "i".

Waitalia ya kwanza wakaendelea kutumia alama kwa aina ya "u" lakini pia "v" kama ilikuwa mwanzoni wa neno. Waroma walipokea vile.

Katika lugha za Ulaya zinazotumia alfabeti ya Kilatini kuna lugha kadhaa zisizo na W kwa sababu hawaihitaji. Katika Kijerumani W hutumiwa kwa sauti ya "V" ya Kiswahili. Kiingezera hutamka kama Kiswahili.