Nenda kwa yaliyomo

E

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Alfabeti ya Kilatini
(kwa matumizi ya Kiswahili)
Aa Bb Cc ch Dd
Ee Ff Gg Hh Ii Jj
Kk Ll Mm Nn Oo Pp
Qq Rr Ss Tt Uu Vv
Ww Xx Yy Zz

E ni herufi ya 11 katika katika alfabeti ya Kilatini ambayo ni pia mwandiko wa Kiswahili cha kisasa. Asili yake ni Epsilon ya alfabeti ya Kigiriki.

Maama za E[hariri | hariri chanzo]

  • Katika shule za nchi mbalimbali E ni maksi ya duni inayoonyesha mtu ameshindwa mtihani.
  • katika muziki E ni noti.
  • Kwa magari E ni alama ya kimataifa ya gari kutoka Hispania ("Espana").
  • *katika fizikia E ni alama ya kiwango cha nishati (E=mc2).

Historia ya alama E[hariri | hariri chanzo]

Kisemiti asilia
mtu anaomba "H"
Kifinisia
H
Kigiriki
Epsilon "E"
Kietruski
E
Kilatini
E
Roman E

Asili ya herufi E ni katika miandiko iliyotangulia alfabeti ya Kilatini. Waroma walipokea mwandiko kutoka alfabeti ya Kigiriki kupitia alfabeti za Kiitalia za awali kama Kietruski. Wagiriki walipokea kutoka Wafinisia.

Wafinisia walikuwa na he iliyokuwa kiasili picha iliyorahisishwa ya mtu anayeomba wakitumia alama tu kwa sauti ya "h". Wagiriki walipochukua alama za Kifinisia walihitaji zaidi alama za vokali lakini siyo ya "h". Kwa hiyo sauti ya alama ikabadilika kuwa "e" na kuitwa epsilon yaani "e ndogo" tofauti na alama ai zilikuwa na matamshi yaleyale.

Witalia na Waroma wa Kale walipokea alama vile kwa kutaja sauti ya "e".