Kichaka

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Kichaka ya Tamarix Aphylla (nchini Israel)
Kichaka cha Aralia Spinosa, Marekani
Kichaka cha Buxus sempervirens, nchi za Mediteranea

Kichaka ni mmea wa kudumu mwenye shina la ubao lakini tofauti na mti kina mashina zaidi ya moja. Tofauti nyingine ni urefu wake ilhali vichaka kwa kawaida huwa na urefu wa sentimita kadhaa hadi mita 6 hivi.

Mimea mingi huweza kutokea ama kama kichaka au kama mti kutegemeana na mazingira yake. Kuna aina za miti mikubwa ambayo, ikikatwa, hukua tena kwa umbo la vichaka.

Vichaka mbalimbali ni muhimu kiuchumi na kulimwa na binadamu kam vile mchai, mbuni na vichaka vingi vya matunda ya kuliwa.