Kipanya manyoya-magumu
Kipanya manyoya-magumu | ||||||||||||||||
---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
Kipanya manyoya-magumu tumbo-kutu (Lophuromys kapusi)
| ||||||||||||||||
Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
| ||||||||||||||||
Ngazi za chini | ||||||||||||||||
Spishi 21:
|
Vipanya manyoya-magumu ni wanyama wagugunaji wa jenasi Lophuromys katika nusufamilia Deomyinae ya familia Muridae. Manyoya yao ni magumu lakini siyo kama yale ya vipanya-miiba. Wanatokea katika Afrika kusini kwa Sahara tu, mara nyingi milimani.
Maelezo
[hariri | hariri chanzo]Vipanya hao wamepata jina lao kwa sababu wana manyoya magumu. Yanafanana na nywele za brashi nyororo lakini hayafanani na [[mwiba}miiba]] kama manyoya ya vipanya-miiba. Mwonekano wao si wa kawaida kwa sababu kadhaa. Rangi ya manyoya inatofautiana kulingana na spishi; inaweza kuwa hudhurungi au kijivukijani hadi kahawia iliyoiva. Spishi fulani huwa na mng'ao zambarau na nyingine zina madoa. Upande wa chini ni rangi ya kutu, ya machungwa, ya kahawa au ya maziwa.
Hawa ni vipanya wanene wenye miguu mifupi kiasi. Urefu wa mwili ni kati ya sm 8 na 17.5 na wa mkia sm 6-10.
Wengi sana wa wanyama hawa wana makovu, masikio yenye mikato au/na mkia unaokosa sehemu. Ngozi yao ni nyembamba na wanaonekana kutumia hii kama maarifa ya kuzuia mbuai. Mkia huvunjika kwa urahisi kusudi mnyama achopoke. Ukiwa umepoteza haukui tena. Ngozi hupasuka kwa urahisi, haswa katika sehemu zifaazo kama vile kisogo. Kwa ukweli, ikiwa mnyama ameshikwa kwa kisogo, anaweza kujikomboa kwa njia ya kujikonyoa akiacha kiraka cha ngozi pamoja na manyoya. Mifano inayopatikana kwenye makumbusho inaonekana nadra ikikosa mipasuko yaliyoshonwa.
Vipanya manyoya-magumu huishi peke yao na wameripotiwa kupigana wakiwekwa pamoja. Hii inaweza kuchangia vidonda vinavyoonwa kwenye wanyama hao.
Imeandikwa kwamba kipanya manyoya-magumu mmoja ameishi kwa muda wa miaka 3 kifungoni.
Makazi na chakula
[hariri | hariri chanzo]Vipanya manyoya-magumu huonekana kuhitaji maeneo manyevu na labda nyasi. Kwa kawaida hawapatikani katika savana kavu na misitu yenye mfuniko mzito wa majani. Hukiakia mchana au usiku au hata alasiri na alfajiri kulingana na spishi.
Chakula chao kina maada nyingi za wanyama kuliko takriban panya wote. Uwiano wa maada za wanyama katika mlo wao ni 40-100% kulingana na spishi. Huu unajumuisha sisimizi, wadudu na invertebrata wengine, vertebrata wadogo, mizoga na maada za mimea.
Spishi
[hariri | hariri chanzo]- Lophuromys angolensis (Angolan brush-furred mouse)
- Lophuromys ansorgei, Kipanya manyoya-magumu wa Ansorge (Ansorge's brush-furred mouse) – Kenya, Tanzania, Uganda
- Lophuromys aquilus, Kipanya manyoya-magumu kijivu (Grey brush-furred mouse) – Burundi, Kenya, Rwanda, Tanzania, Uganda
- Lophuromys brevicaudus (Short-tailed brush-furred rat)
- Lophuromys brunneus (Brown brush-furred mouse)
- Lophuromys chercherensis ( Chercher Mountains brush-furred mouse)
- Lophuromys chrysopus (Ethiopian forest brush-furred mouse)
- Lophuromys dieterleni (Dieterlen's brush-furred mouse)
- Lophuromys dudui (Dudu's brush-furred rat)
- Lophuromys eisentrauti (Eisentraut's brush-furred rat)
- Lophuromys flavopunctatus (Yellow-spotted brush-furred rat)
- Lophuromys huttereri (Hutterer's brush-furred mouse)
- Lophuromys kilonzoi, Kipanya manyoya-magumu wa Kilonzo (Kilonzo's brush-furred mouse)
- Lophuromys luteogaster (Yellow-bellied brush-furred rat)
- Lophuromys machangui, Kipanya manyoya-magumu wa Ml. Rungwe ( Machangu's brush-furred rat)
- Lophuromys makundii, Kipanya manyoya-magumu wa Ml. Hanang (Makundi's brush-furred mouse)
- Lophuromys margarettae, Kipanya manyoya-magumu wa Margaretta ( Margaretta's brush-furred rat) – Kenya, Tanzania
- Lophuromys medicaudatus, Kipanya manyoya-magumu mkia-mfupi (Medium-tailed brush-furred rat) – Rwanda
- Lophuromys melanonyx (Black-clawed brush-furred rat)
- Lophuromys menageshae (Menagesha brush-furred mouse)
- Lophuromys nudicaudus (Fire-bellied brush-furred rat)
- Lophuromys pseudosikapusi (False rusty-bellied brush-furred rat)
- Lophuromys rahmi, Kipanya manyoya-magumu wa Rahm (Rahm's brush-furred rat) – Rwanda
- Lophuromys rita (Rita's brush-furred rat)
- Lophuromys roseveari (Mount Cameroon brush-furred rat)
- Lophuromys sabunii, Kipanya manyoya-magumu wa Ufipa (Sabuni's brush-furred mouse)
- Lophuromys sikapusi (Rusty-bellied brush-furred rat)
- Lophuromys simensis (Simien brush-furred rat)
- Lophuromys stanleyi, Kipanya manyoya-magumu wa Ruwenzori (Stanley's brush-furred mouse) – Uganda
- Lophuromys verhageni, Kipanya manyoya-magumu wa Ml. Meru (Verhagen's brush-furred mouse)
- Lophuromys woosnami, Kipanya manyoya-magumu wa Woosnam (Woosnam's brush-furred rat) – Burundi, Rwanda, Uganda
- Lophuromys zena, Kipanya manyoya-magumu wa Zena (Zena's brush-furred rat) – Kenya