Nenda kwa yaliyomo

Kiribati

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ribaberikin Kiribati
Jamhuri ya Kiribati
Bendera ya Kiribati Nembo ya Kiribati
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Te Mauri, Te Raoi ao Te Tabomoa
(Afya, amani na usitawi)
Wimbo wa taifa: Teirake Kaini Kiribati
Lokeshen ya Kiribati
Mji mkuu Teinainano (Tarawa)
1°28′ N 173°2′ E
Mji mkubwa nchini Betio (Tarawa)
Lugha rasmi Kiingereza , Kikiribati
Serikali Jamhuri
Taneti Maamau
Uhuru
kutoka Uingereza

12 Julai 1979
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
726 km² (ya 186)
0
Idadi ya watu
 - Julai 2005 kadirio
 - 2010 sensa
 - Msongamano wa watu
 
103,500 (ya 197)
103,500
135/km² (ya 73)
Fedha Dollar ya Australia (AUD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC+12, +13, +14)
(UTC)
Intaneti TLD .ki
Kodi ya simu +686

-

1 Supplemented by a nearly equal amount from external sources.


Kiribati ni nchi ya visiwani ya Polynesia na Mikronesia katika Pasifiki karibu na ikweta yenye wakazi 100,000 hivi.

Eneo lake ni visiwa 33 vilivyosambaa kwa 5,200,000 km². Visiwa 32 vimepangwa katika vikundi vinne:

Mji mkuu wa Bairiki uko kwenye kisiwa cha Tarawa.

Ramani ya Kiribati

Jiografia

[hariri | hariri chanzo]

Kiribati ina eneo pana sana; umbali kati ya kisiwa cha magharibi kabisa cha Banaba hadi kisiwa cha mashariki kabisa cha Millenium ni kilomita 4,835; umbali wa kaskazini-kusini ni km. 1,973.

Eneo hili liko katikati ya Hawaii na Australia.

Karibu visiwa vyote havipiti kimo cha mita 2 juu ya UB. Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa duniani na kupanda kwa uwiano wa bahari wataalamu wamekadiria ya kwamba nchi itazama kabisa katika hii karne ya 21.

Lugha na dini

[hariri | hariri chanzo]

Kuna lugha mbili tu nchini Kiribati, zote mbili zikiwa lugha rasmi, yaani Kiingereza na hasa Kikiribati.

Upande wa dini, linaongoza Kanisa Katoliki (56%), likifuatwa na madhehebu mbalimbali ya Uprotestanti.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]


Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.