Nenda kwa yaliyomo

Kassim Majaliwa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Kassim Majaliwa Majaliwa)
Kassim Majaliwa


Waziri Mkuu wa Tanzania
Aliingia ofisini 
19 Novemba 2015

tarehe ya kuzaliwa 22 Desemba 1960 (1960-12-22) (umri 64)
Ruangwa
utaifa Mtanzania
chama Chama Cha Mapinduzi
mhitimu wa chuo cha ualimu Mtwara
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
Chuo Kikuu cha Stockholm
taaluma mwanasiasa nchini Tanzania
Fani yake Mwalimu

Kassim Majaliwa (alizaliwa 22 Disemba 1960) ni mwanasiasa nchini Tanzania na waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Majaliwa ni mwenyeji wa Mnacho katika Wilaya ya Ruangwa aliposoma shule ya msingi kati ya mwaka 1970 hadi 1976. Akaendelea kusoma kwenye Shule ya Sekondari Kigonsera hadi 1980.

Miaka 1984-1986 alifanya kazi ya ualimu huko Lindi na tangu 1988 aliajiriwa na wizara ya elimu. Mwaka 1991 akajiunga na chuo cha ualimu Mtwara akaendelea na masomo ya digrii ya kwanza kwenye Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, masomo ya digrii ya pili kwenye Chuo Kikuu cha Stockholm (Uswidi) aliyomaliza 1999.

Mwaka 2000 alipewa kazi ya Mkuu wa Wilaya.

Alikuwa kwanza mbunge wa jimbo la Ruangwa tangu mwaka 2010 akigombea kwa CCM.

Aliwahi kushika vyeo vya naibu waziri wa utawala wa mikoa na serikali ya mitaa katika ofisi ya waziri mkuu tangu mwaka 2010[1] [2]na mkuu wa mkoa wa Lindi kuanzia 2006 hadi 2010.

Tarehe 19 Novemba 2015 aliteuliwa na rais John Magufuli kuwa waziri mkuu wa serikali ya awamu ya tano nchini Tanzania.[3]

Ni mpenzi wa michezo ya klabu za Tanzania na ni shabiki wa Simba S.C..

  1. "Member of Parliament CV". Parliament of Tanzania. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2015-07-22. Iliwekwa mnamo 24 Februari 2013. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)
  2. "Taaarifa juu ya uteuzi wa Majaliwa kuwa Waziri mkuu katika gazeti la Mwananchi, 19 Novemba 2015". Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-05-15. Iliwekwa mnamo 2015-11-19. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)
  3. "JPM names Kassim Majaliwa Prime Minister". THE CITIZEN. Ilihifadhiwa kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2019-06-11. Iliwekwa mnamo 19 Novemba 2015. {{cite web}}: Unknown parameter |= ignored (help)CS1 maint: date auto-translated (link)

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Ofisi za Kisiasa
Alitanguliwa na
Mizengo Kayanza Peter Pinda
Waziri Mkuu wa Tanzania
2015-
Akafuatiwa na
[[]]