Yohane Ogilvie

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka John Ogilvie)
Mt. John Ogilvie
Kifodini cha Mt. John Ogilvie.

John Ogilvie (Drumnakeith, Banffshire, 1579Glasgow Cross, 10 Machi 1615) alikuwa padri Mjesuiti kutoka Uskoti.

Mtoto wa kwanza wa Walter Ogilvie, Mkalvini tajiri, alipokuwa na umri wa miaka 12 alitumwa Ulaya bara kwa masomo.

Mwaka 1596 alijiunga na Kanisa Katoliki huko Leuven, Ubelgiji, na miaka mitatu baadaye alijiunga na Shirika la Yesu.

Alipata upadrisho huko Paris, Ufaransa, mwaka 1610. Akifanya uchungaji huko Rouen, Normandy, aliomba mara kadhaa kutumwa Glasgow (ingawa tangu mwaka 1560 huko Uskoti ilikuwa marufuku kutetea Ukatoliki).[1]

Alipokosa msaada huko, alikwenda London, Uingereza, tena Paris, na mnamo Novemba 1613 akarudi Uskoti akijidai ni mfanyabiashara na kutumia jina la John Watson. Kumbe alianza kufanya utume kwa bidii akihubiri na kusoma Misa kwa siri hadi Oktoba 1614, alipofungwa gerezani chini ya mfalme James VI.

Hatimaye alinyongwa na kukatwa vipandevipande.[2]

Alitangazwa mwenye heri mwaka 1929 na mtakatifu mwaka 1976.[3]

Sikukuu yake huadhimishwa na Wakatoliki tarehe 10 Machi[4].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. "Patron Saints Index: Saint John Ogilvie". 2009-01-15. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 15 January 2009. Iliwekwa mnamo 2017-05-14.  Unknown parameter |df= ignored (help); Check date values in: |archivedate= (help)
  2. "10. mars: Den hellige John Ogilvie (~1580-1615)". 2010-03-13. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 13 March 2010. Iliwekwa mnamo 2017-05-14.  Unknown parameter |df= ignored (help); Check date values in: |archivedate= (help)
  3. "Irondequoit Catholic Communities - - John Ogilvie". 2008-10-11. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 11 October 2008. Iliwekwa mnamo 2017-05-14.  Unknown parameter |df= ignored (help); Check date values in: |archivedate= (help)
  4. Martyrologium Romanum

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.