Ipinda

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Kata ya Ipinda
Kata ya Ipinda is located in Tanzania
Kata ya Ipinda
Kata ya Ipinda

Mahali pa Ipinda katika Tanzania

Majiranukta: 9°29′0″S 33°54′0″E / 9.48333°S 33.90000°E / -9.48333; 33.90000
Nchi Tanzania
Mkoa Mbeya
Wilaya Kyela
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 27,665

Ipinda ni kata ya Wilaya ya Kyela katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania.

Kata ya Ipinda inaundwa na vijiji vya Ipinda, Ikulu, Kafundo, Kisale, Bujela, Mabunga, Kanga, Ikumbilo, Kingili na Lupaso.

Kata ya Ipinda ina mito kama vile mto Lufilyo, mto Kanga, mto Ngugwisi, mto Kasyabone na mto Ipinda.

Pia, kata hiyo ina ziwa lenye asili ya volkano liitwalo ziwa Kingili.

Msimbo wa posta ni 53711.

Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 27,665 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 20,847 [2] walioishi humo.

Ipinda inakaliwa na jamii ya Wanyakyusa waishio kaskazini mwa ziwa Nyasa ikiwa kama jamii tawala. Pia imechanganyika na watu waliohamia humo kutoka makabila mbalimbali kama vile Wakinga, Wangoni, Wahehe.

Wakazi hao hujishughulisha hasa na kilimo cha mpunga kikiwa kama kilimo kikuu kwao kwani wanalitegemea zao hilo kwa chakula na biashara. Pia, wakazi wa Ipinda wanazalisha michikichi na kakao kama mazao ya biashara.

Pamoja na hayo Ipinda ni kata yenye huduma mbalimbali za kijamii kama vile kituo cha afya kikubwa kifahamikacho kama kituo cha afya Ipinda, pia Ipinda ina shule tatu za sekondari amabazo ni Ipinda, Dinnob na Kafundo. Zile za msingi ni Ipinda, Mwenge, Ikilu, Jitegemee, Kafundo, Kanga, Kisale, Lupaso na Mabunga.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz
  2. "Sensa ya 2012, Mbeya - Kyela DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2004-01-02. Iliwekwa mnamo 2017-03-12. 
Kata za Wilaya ya KyelaMkoa wa Mbeya - Tanzania

Bondeni | Bujonde | Busale | Ibanda | Ikama | Ikimba | Ikolo | Ipande | Ipinda | Ipyana | Itope | Itunge | Kajunjumele | Katumbasongwe | Kyela | Lusungo | Mababu | Makwale | Matema | Mbugani | Mikoroshoni | Muungano | Mwanganyanga | Mwaya | Ndandalo | Ndobo | Ngana | Ngonga | Njisi | Nkokwa | Nkuyu | Serengeti | Talatala


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Ipinda kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.