Ndandalo
Ndandalo ni kata ya Wilaya ya Kyela katika Mkoa wa Mbeya, Tanzania. Inapitiwa na mto unaokwenda kumwaga maji katika ziwa Nyasa.
Katika sensa iliyofanyika mwaka 2022 wakazi walihesabika kuwa 8,768 [1].
Ndandalo ni kata ambayo inachangia kiasi kikubwa cha mapato katika wilaya ya Kyela.
Ina viwanda vikubwa na vidogo vikiwemo viwanda vya sabuni, mafuta, kuchonga vyuma, usindikaji wa vyakula na kadhalika.
Ndandalo ina machinjio ya wanyama yanayotegemewa na wilaya.
Ina shule za msingi mbili ambazo ni shule ya msingi Ndandalo na shule ya msingi Mbogela.
Ndandalo ina vyuo viwili ambavyo kimoja ni Kyela Politechnic College (KPC) na Chuo cha Ufundi.
Ndandalo ina vituo vya redio viwili ambavyo ni Kyela FM na Keifo FM.
Ndandalo ina viwanja viwili vikubwa vya mpira na kiwanja cha kuchezea tamaduni za Kinyakyusa.
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]Kata za Wilaya ya Kyela – Mkoa wa Mbeya - Tanzania | ||
---|---|---|
Bondeni | Bujonde | Busale | Ibanda | Ikama | Ikimba | Ikolo | Ipande | Ipinda | Ipyana | Itope | Itunge | Kajunjumele | Katumbasongwe | Kyela | Lusungo | Mababu | Makwale | Matema | Mbugani | Mikoroshoni | Muungano | Mwanganyanga | Mwaya | Ndandalo | Ndobo | Ngana | Ngonga | Njisi | Nkokwa | Nkuyu | Serengeti | Talatala |
Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Mbeya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Ndandalo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno. |