Nenda kwa yaliyomo

Gatundu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Gatundu
Nchi Kenya
Kaunti Kaunti ya Kiambu
Wilaya Wilaya ya Gatundu
Eneo bunge Gatundu Kusini
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 20,000 (haijahakikishwa)
Mji wa Gatundu

Gatundu ni mji uliopo eneo la kati la Kenya katika Kaunti ya Kiambu. Mji huu una umaarufu kwa kuwa rais wa kwanza wa Kenya, Jomo Kenyatta na mwana wake rais Uhuru Kenyatta, waliishi karibu na hapa. Unapatikana juu ya kilima kilichozingirwa na Mto Thiririka na Mto Muthurumbi.

Mji huu uko chini ya utawala wa serikali ya Kaunti. Gatundu ndio makao makuu ya eneo bunge la Gatundu Kusini na kaunti ndogo ya Gatundu Kusini.

Mbunge wa eneo hili ni Moses Kuria (pia MK). Rais wa sasa wa Jamuhuri ya Kenya, Uhuru Muigai Kenyatta, alikuwa mbunge wa eneo hili miaka 2002-2013.

Mahakama ya Gatundu yapatikana karibu na Hospitali ya Wilaya ya Gatundu. Ilifunguliwa mwaka 2014.

Soko la Gatundu

Shughuli kuu ya kiuchumi ni uuzaji wa bidhaa. Soko lenye maghorofa mawili huwa linavutia wafanyabiashara kutoka vijiji vinavyozunguka mji huu. Vijiji hivi hukuza bidhaa za kilimo ambazo huchangia katika uchumi wa eneo hili.

Hospitali ya Ngazi ya 4 ya Gatundu huhudumia kanda ya Gatundu Kusini na Kaskazini. Upanuzi wa hospitali ulifanywa kati ya mwaka 2013 hadi Aprili 2016 ambapo jengo mpya liliadhimishwa na Rais Uhuru. Jengo hili lina vitanda 12 vya huduma ya dharura, vitanda 84, maabara, kitengo cha uzazi, thieta ya upasuaji, wadi, skana za CT, eksirei na lifti nne. Lilijengwa kwa usaidizi wa Uchina.

Hospitali nyingine zinazopatikana Gatundu ni pamoja na:

  • St. Jude Nursing Home
  • St. Mary's International Hospital

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu: