Mauzo

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Jump to navigation Jump to search

Mauzo ni shughuli inayohusiana na kuuza au kiasi cha bidhaa au huduma zinazouzwa katika muda fulani.

Muuzaji humaliza kitendo cha uuzaji baada ya kujibu mwito wa ununuzi. Kuna kupitisha umiliki wa bidhaa na kulipa, ambapo kuna makubaliano ya bei ambayo italipiwa bidhaa ile. Muuzaji ndiye anayefanya tendo lile la uuzaji na uzo lile laweza kumalizika kabla ya mnunuzi kumaliza kulipa. 

Ufafanuzi[hariri | hariri chanzo]

Mtu au shirika linaloonyesha nia ya kupata bidhaa ya thamani inayotolewa linajulikana kama mnunuzi au mteja mtarajiwa. Kununua na kuuza ni lile tendo la kubadilishana umiliki. Kununua ni kupokea umiliki wa kinacho uzwa ilhali kuuza ni kupitisha umiliki kwake mnunuzi baada ya malipo. Muuzaji na mnunuzi huafikiana ili kukamilisha ubadilishaji wa thamani.[1]

Katika mauuzo kunaweza kuwa na kujadiliana bei au bei inaweza kuwa isio batirika. Sana sana bei ya bidhaa au huduma huukuliwa na haja ya wanunuzi na wingi wake sokoni. Kwa biashara zinazolenga wanunuzi fulani hasa matajiri muuzaji anaweza kuiweka bei ya bidhaa bila kuzingatia bei ya ile bidhaa au huduma sokoni. [2]

Mbinu[hariri | hariri chanzo]

Mauzo yanaweza kuwa au kupitia:[3]

 • Mauzo ya moja kwa moja
 • Mauzo yasiyo ya moja kwa moja
 • Mawakala
 • Rejareja
 • Ombi la pendekezo
 • Biashara kwa biashara[4]
 • Ya kielektroniki

Mawakala wa mauzo[hariri | hariri chanzo]

Mawakala katika mchakato wa mauzo anaweza kuwakilisha upande wowote katika mchakato wa mauzo; kwa mfano:

 1. Wakala wa mauzo
 2. Wakala mnunuzi
 3. Wakala anayewakilisha pande zote mbili
 4. Wakala wa kuangalia shughuli tu
 5. Uwakilishi wa nje wa mambo ya mauzo
 6. Msimamizi wa mauzo wa kutekeleza mikakati ya mauzo na kuratibu idara ya mauzo
 7. Mfanyabiashara muuzaji
 8. Wataalamu wa mauzo mtandaoni

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

 1. Putthiwanit, C.; Ho, S.-H. (2011). "Buyer Success and Failure in Bargaining and Its Consequences". Australian Journal of Business and Management Research 1 (5): 83–92.
 2. Halder Salim (27 June 2018). High Ticket Pricing and Markets (en-US). Iliwekwa mnamo 24 July 2018.
 3. (n.d.) Compendium of Professional Selling. United Professional Sales Association. 
 4. John, Bryson (10 Feb 2003). "What To Do When Stakeholders Matter: A Guide to Stakeholder Identification and Analysis Techniques". London School of Economics and Political Science. http://cep.lse.ac.uk/seminarpapers/10-02-03-BRY.pdf.
ThreeCoins.svg Makala hii kuhusu mambo ya uchumi bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mauzo kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.