Eugen Mwaiposa

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Eugen Elishiringa Mwaiposa (23 Novemba 1960 - 2 Juni 2015) alikuwa mwanasiasa wa kike wa CCM wa Tanzania na Mbunge wa jimbo la Ukonga kutoka 2010 hadi 2015. [1]

Elimu[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa katika Mkoa wa Kilimanjaro akaanza elimu yake katika shule ya msingi ya Nkweseko 1967-1974. Alihitimu shule ya upili mnamo 1985 katika Shule ya Biashara Shinyanga (Shycom).

Alihitimu kwenye Chuo Kikuu cha Uchumi wa Kitaifa na Uchumi wa Dunia, iliyojulikana hapo awali kama Taasisi ya Uchumi wa Juu "Karl Marx", huko Sofia, Bulgaria ambapo alipata shahada yake katika Uchumi wa Kimataifa mnamo 1986 hadi 1992. Kwenye Chuo Kikuu cha Strathclyde huko Glasgow, Uskoti, alipokea shahada ya uzamili mnamo 2007.

Kabla ya kujiunga na siasa[hariri | hariri chanzo]

Kabla ya kujiunga na siasa, Mwaiposa alifanya kazi kwa matawi tofauti ya benki ya CRDB jijini Dar es Salaam kutoka 1986 hadi 2008.

Mwaiposa alikuwa mjasiriamali ambaye aliamini katika kuwapa wanawake maskini fursa ya kuanza biashara ndogondogo kwa wenyewe. Alikuwa mwenyekiti wa Kipunguni SACCOSS ambayo kusudi lake la pekee lilikuwa kutoa mikopo kwa watu au kikundi cha watu wanaohitaji mtaji na pia ilifanya kama benki kupata pesa kwa jamii.

Alifariki mnamo 2015. [2] [3]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. "Member of Parliament CV". Parliament of Tanzania. 2010. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 3 November 2013. Iliwekwa mnamo 4 September 2013.  Check date values in: |archivedate=, |accessdate= (help)
  2. Eugene Mwaiposa afariki dunia EATV
  3. Tears as MP Eugen Mwaiposa dies Archived 9 Juni 2015 at the Wayback Machine. Daily News
Makala hii kuhusu mwanasiasa fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Eugen Mwaiposa kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.