Embakasi
Embakasi ni mtaa wa Nairobi, mji mkuu wa Kenya. Uko mashariki mwa katikati ya jiji. Ni mtaa wa makazi na wengi wa raia wanaoishi humo ni wa mapato ya daraja la pili la wastani. Ni kata ya eneo bunge la Embakasi Mashariki, kaunti ya Nairobi.
Uwanja wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta, uwanja wa ndege mkuu Nairobi uko Embakasi na ulijulikana kama Embakasi Airport wakati ulipofunguliwa mwaka wa 1958.
Tarafa ya Embakasi
[hariri | hariri chanzo]Embakasi pia ni jina la utawala la tarafa mjini Nairobi. Imegawanywa katika maeneo yafuatayo (sensa ya 1999)[1]
- Dandora
- Embakasi
- Kariobangi South
- Kayole
- Mukuru Kwa Njenga
- Njiru
- Ruai
- Umoja
Tukio
[hariri | hariri chanzo]Katika masaa ya asubuhi ya 27 Januari 2008, Mbunge wa Eneo Bunge la Embakasi, Mugabe Were alipigwa risasi na washambulizi wawili na kufa. Kulingana na taarifa za habari, Mugabe alikuwa tu amewasili katika boma yake wakati aliposhambuliwa akiwa bado katika gari lake, kabla ya lango kufunguliwa. Mugabe alichaguliwa kuwa mjumbe wa Orange Democratic Movement, chama cha upinzani nchini Kenya. Uvumi kuhusu uwezekano wa mauaji haya kuwa ya kisiasa bado unazingira kifo hiki katika mgogoro uliotokea kuhusu uchaguzi wa rais wa tarehe 27 Desemba 2007[2][3].
Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- ↑ International Livestock Research Institute: Urban Poverty Estimates For Kenya's Provinces, Districts, Kitengo na Locations Ilihifadhiwa 18 Julai 2011 kwenye Wayback Machine.
- ↑ http://www.reuters.com/article/worldNews/idUSWAL22103220080129
- ↑ http://news.bbc.co.uk/2/hi/africa/7214558.stm
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]1°18′S 36°55′E / 1.300°S 36.917°E
Makala hii kuhusu maeneo ya Kenya bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Embakasi kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |