Panya-vinamasi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Dasymys)
Panya-vinamasi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Mamalia (Wanyama wenye viwele wanaonyonyesha wadogo wao)
Oda: Rodentia (Wanyama wagugunaji)
Nusuoda: Myomorpha (Wanyama kama panya)
Familia: Muridae (Wanyama walio na mnasaba na panya)
Nusufamilia: Murinae (Wanyama wanaofanan na vipanya-miiba)
Jenasi: Dasymys
Peters, 1875
Ngazi za chini

Spishi 11:

Panya-vinamasi ni wanyama wagugunaji wa jenasi Dasymys katika nusufamilia Murinae ya familia Muridae ambao wanatokea Afrika kusini kwa Sahara katika vinamasi na maeneo manyevu mengine yenye nyasi ndefu nyingi, mara nyingi kwenye miinuko.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Panya hao wanaonekana kuwa wenye nguvu na manyoya marefu. Wana uso bapa kiasi na masikio pinki ya mviringo. Urefu wa mwili ni sm 12-19, urefu wa mkia sm 10-18 na uzito ni g 80-165. Nyayo zao ni ndefu. Manyoya ni kahawia iliyoiva hadi meusi lakini meupe upande wa chini.

Haijulikani sana juu ya mwenendo wa panya-vinamasi kwa sababu ya ugumu wa kunasa vielelezo hai na tabia yao ya kuishi katika vikundi vidogo vilivyotengwa. Panya-vinamasi hujulikana kujenga viota tata ili kubaki wakilindwa wakati wa kunyonyesha wachanga wao. Hukiakia usiku ingawa wengine walionekana wakati wa mchana. Huishi ardhini lakini huingia maji mara nyingi na kwa kawaida huchimba vishimo vyao kando ya kingo za mito vinavyopita sambamba na mto au kuuelekea moja kwa moja. Panya-vinamasi wanaweza kuogelea vizuri na hata kuogelea kupitia vishimo vyao, wakati vimejaa maji.

Lishe ya panya-vinamasi kimsingi imeundwa na dutu ya mimea kijani. Walakini, vielelezo vingine vimeonekana na wadudu kwenye yaliyomo ndani ya tumbo pia. Lakini hula mimea hasa. Kwa kawaida hutegemea mashina na vichwa vya nyasi na matete yanayokua majini karibu na vishimo vyao.

Spishi[hariri | hariri chanzo]