Kisawe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Kisawe ni neno lenye maana ileile ya neno lingine; kwa mfano jogoo kisawe chake ni kikwara, bamia kisawe chake ni binda na mengineyo, kama vile nyanya-bibi, tembo-ndovu, mtu–mja-adinasi-mahuluki-insi-binadamu, rafiki–msena-mwandani-bui, ugonjwa-maradhi.

Katika sentensi kisawe kimoja kinaweza kubadilishwa na kisawe kingine bila kubadilisha maana ya sentensi.

Hayo maneno yaliyo na maana sawa au yanayokaribiana sana kimaana yanaonyesha utajiri wa lugha fulani na huwezesha kuremba sentensi, mazungumzo na maandishi viwe vya uzuri wa kifasihi.

Makala hii kuhusu mambo ya lugha bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Kisawe kama historia yake, uenezi au maendeleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.