Danieli (Biblia)
Danieli (kwa Kiebrania na Kiaramu דָּנִיֵּאל – dāniyyēl) ni mhusika mkuu wa Kitabu cha Danieli kwenye Biblia. Wayahudi wanamwona kama mtu mwenye hekima kubwa, Wakristo na Waislamu wanamjua kama nabii.
Katika simulizi la Kitabu cha Danieli yeye ni kijana Myahudi kutoka Yerusalemu anayekamatwa na mfalme Nebukadreza pamoja na wakazi wengine wa mji na kupelekwa uhamishoni Babeli. Hapo anamhudumia mfalme na wafuasi wake hadi wakati wa mfalme Koreshi wa Uajemi anayeshinda Babeli na kuwapa Wayahudi uhuru wao tena.
Wataalamu wa siku hizi wanaona kwamba kitabu si taarifa ya kihistoria bali masimulizi ya kishairi yaliyotungwa karne kadhaa baadaye katika mazingira ya mashambulizi ya wafalme Wagiriki katika nchi ya Israeli. Uwezekano mkubwa ni kwamba Danieli hakuwa mtu wa kihistoria bali mhusika katika masimulizi yanayolenga kujenga imani katika mazingira ya kiadui.
Hata hivyo, kuna miji sita ambako wenyeji wanaonyesha kaburi la Danieli. Maarufu zaidi liko huko Shushani, kusini mwa Iran.
Jina la Danieli linamaanisha "Mungu (El) ndiye hakimu wangu". Pamoja na huyo Danieli, mhusika katika kitabu chake, Biblia inataja watu walioitwa kwa jina hilo kwenye nafasi tatu nyingine:
- Kitabu cha Ezekieli (14:14, 14:20 na 28: 3) kinamrejelea Danieli mmoja mashuhuri aliyejulikana kwa hekima na haki. Katika aya ya 14:14, Ezekieli anasema juu ya nchi yenye dhambi ya Israeli kwamba "wajapokuwa watu hawa watatu, Nuhu, na Danieli, na Ayubu, kuwamo ndani yake, wangejiokoa nafsi zao wenyewe tu kwa haki yao". Katika sura ya 28, Ezekieli anamdhihaki mfalme wa Tiro, akiuliza kwa maneno ya kejeli, "wewe una hekima kuliko Danieli?" Kama kitabu cha Danieli si cha kihistoria, basi mwandishi wake anaonekana alichukua sura hii ya hadithi, mashuhuri kwa hekima yake, kutumika kama mhusika wake mkuu.
- Ezra 8: 2 inamtaja kuhani aliyeitwa Danieli ambaye alitoka Babeli kwenda Yerusalemu na Ezra.
- Daniel alikuwa mwana wa mfalme Daudi aliyetajwa kwenye 1 Mambo ya Nyakati 3: 1.
Marejeo[hariri | hariri chanzo]
Vitabu juu yake[hariri | hariri chanzo]
- Collins, John J. (1984). Daniel: With an Introduction to Apocalyptic Literature. Eerdmans. ISBN 9780802800206.
- Collins, John J. (1999). "Daniel", Dictionary of Deities and Demons in the Bible. Eerdmans. ISBN 9780802824912.
- Coogan, Michael (2008). The Old Testament: A Very Short Introduction. Oxford University Press. ISBN 9780199719464.
- Day, John (1980). "The Daniel of Ugarit and Ezekiel and the Hero of the Book of Daniel". Vetus Testamentum 30 (2): 174–184.
.
- Doukhan, Jacques (2000). Secrets of Daniel: Wisdom and Dreams of a Jewish Prince in Exile. Review and Herald Pub Assoc. ISBN 9780828014243.
- Ginzberg, Louis (1998). The Legends of the Jews 4. JHU Press. ISBN 9780801858932.
- (1906) "Daniel's Tomb", Jewish Encyclopedia.
- Miller, Stephen R. (1994). Daniel. B&H. ISBN 9780805401189.
- (2002) Historical Dictionary of Prophets in Islam and Judaism. Scarecrow Press. ISBN 9780810866102.
- Redditt, Paul L. (2008). Introduction to the Prophets. Eerdmans. ISBN 9780802828965.
- Reid, Stephen Breck (2000). "Daniel, Book of", Eerdmans Dictionary of the Bible. Eerdmans. ISBN 9789053565032.
- Seow, C.L. (2003). Daniel. Westminster John Knox Press. ISBN 9780664256753.
- Spencer, Richard A. (2002). "Additions to Daniel", The Deuterocanonicals/Apocrypha. Mercer University Press. ISBN 9780865545106.
- Stone, Michael E. (2011). Ancient Judaism: New Visions and Views. Eerdmans. ISBN 9780802866363.
- Towner, Wayne Sibley (1984). Daniel. Westminster John Knox Press. ISBN 9780664237561.
- Walton, John J. (1994). Ancient Israelite Literature in Its Cultural Context. Zondervan. ISBN 9780310365914.
- Wesselius, Jan-Wim (2002). "The Writing of Daniel", The Book of Daniel: Composition and Reception. Brill. ISBN 978-0391041288.
Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]
- Easton, Matthew George (1897). "Daniel" . Kamusi ya Biblia ya Easton (New and revised ed.). T. Nelson na Wanawe.
media kuhusu Daniel (Biblical figure) pa Wikimedia Commons
![]() |
Makala hii kuhusu mambo ya Biblia bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Danieli (Biblia) kama historia yake au athari wake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |