Nyuki-plastiki

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Colletidae)
Nyuki-plastiki
Colletes cunicularius
Colletes cunicularius
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Hymenoptera (Wadudu wenye mabawa mangavu)
Nusuoda: Apocrita (Hymenoptera wenye kiuno chembamba)
Familia ya juu: Apoidea
(bila tabaka): Anthophila
Familia: Colletidae
Lepeletier, 1841
Ngazi za chini

Nusufamilia 5:

Nyuki-plastiki (kutoka Kiing. polyester bees) ni nyuki wadogo wa family Colletidae katika familia ya juu Apoidea ya oda Hymenoptera wanaojenga viota vyao ardhini, hasa katika udongo wenye mchanga, au katika mbao, katikati ya miamba au katika machimbo ya nyungunyungu. Hupaka mnyeso fulani kwa ulimi wao kwenye ukuta wa chimbo. Baada ya kukauka mnyeso huo unafanana na plastiki (poliesta). Spishi za nusufamilia Hylaeinae huitwa nyuki uso-njano mara nyingi. Nyuki hawa ni wapweke, lakini huenda kujenga viota vyao karibu na kila kimoja mpaka mkongamano wa maelfu ya viota. Wanatokea duniani kote, hasa Australia na Amerika ya Kusini, lakini Afrika pia ina spishi nyingi ambazo 21 katika Afrika ya Mashariki.

Maelezo[1][2][hariri | hariri chanzo]

Hao ni nyuki wadogo wa urefu wa mm 2.5-7. Wana ndimi fupi. Spishi za nusufamilia Colletinae zina nywele nyingi kiasi, lakini Hylaeinae zina nywele chache na fupi zaidi. Colletinae ni nyeusi zenye nywele nyeupe, maziwa au njano kuzunguka thoraksi na katika milia kwenye fumbatio. Zina nywele maalum kwenye femuri za nyuma ambazo hukusanya na kushikilia chavua ambazo kwa pamoja huitwa skopa (scopa). Hylaeinae hazina skopa lakini hubeba chavua katika gole lao. Pia ni nyeusi lakini sehemu za mwili, fumbatio hasa, zinaweza kuwa nyekundu huku uso na sehemu za miguu zikiwa njano au maziwa kwa kawaida.

Biolojia[1][2][hariri | hariri chanzo]

Collete cunicularis akichimba chimbo lake.

Majike wa Colletinae huchimba machimbo kwenye udongo tifutifu kiasi ambapo huweka viota vyao. Ingawa kila jike huchimba chimbo lake mwenyewe, mamia hadi maelfu ya machimbo yanaweza kutokea pamoja katika eneo dogo. Chimbo lina shimo kuu lenye matawi mafupi. Kijumba cha kizazi hutengenezwa mwishoni mwa kila tawi kwa usaidizi wa mnyeso kutoka kwa tezi za mate ambao hukauka kwenye tabaka linalofanana na plastiki na kuzuia maji na ukuaji wa kuvu. Vijumba vinatolewa na donge la mchanganyiko wa chavua na mbochi na yai hutagwa juu ya kila donge. Majana wanaoibuka kisha hupata chakula tayari. Baada ya bambuaji nne jana anakuwa bundo, ambamo nyuki mpevu huibuka mwanzoni mwa msimu wa mvua.

Majike wa Hylaeinae hutafuta mashimo yaliyopo ama ardhini, kama machimbo ya nyungunyungu, au katika mbao au katikati ya miamba. Ndani, wanaunda safu moja ya vijumba ambavyo huvipatia maelezi ya kiowevu ya chavua yaliyochanganywa na mbochi. Kama nusufamilia nyingine, kuta za vijumba zimepakwa na mnyeso unaokauka kwenye tabaka linalofanana na plastiki. Vinginevyo, mzunguko wa maisha ni sawa.

Spishi za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

  • Colletes marleyi
  • Colletes opacicollis
  • Colletes rothschildi
  • Colletes rufitarsis
  • Colletes somereni
  • Hylaeus acariphorus
  • Hylaeus cribratus
  • Hylaeus fortis
  • Hylaeus heraldicus
  • Hylaeus magnificus
  • Hylaeus major
  • Hylaeus neavei
  • Hylaeus nyassanus
  • Hylaeus psaenythioides
  • Hylaeus rufipedoides
  • Hylaeus sansibaribius
  • Hylaeus scutispinus
  • Hylaeus subfortis
  • Hylaeus tinctulus
  • Hylaeus ugandicus
  • Hylaeus umtalicus

Picha[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]