Nenda kwa yaliyomo

Klelia Barbieri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Clelia Barbieri)
Picha halisi pekee ya Mt. Klelia.

Klelia Barbieri (kwa Kiitalia Clelia Barbieri; Bologna, 13 Februari 1847 - San Giovanni in Persiceto, 13 Julai 1870) alikuwa msichana wa Italia aliyeshughulikia mema ya kiroho ya wasichana wenzake akaanzisha jumuia ya wanawake waliojiweka wakfu kwa Mungu, ambayo baadaye ikawa shirika la Masista Waminimi wa Bikira Maria wa Mateso ambao wawajibike hasa kwa wale fukara na wenye kuhitaji zaidi[1].

Anahesabiwa kuwa mwanamke mwanzilishi wa utawa mwenye umri mdogo kuliko wote.[2]

Alitangazwa na Papa Paulo VI kuwa mwenye heri tarehe 2 Oktoba 1968, halafu Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu tarehe 9 Aprili 1989.

Anaheshimiwa kama bikira hasa tarehe 13 Julai, ambayo ndiyo sikukuu yake[3].

Klelia alizaliwa na Giuseppe Barbieri, aliyekuwa kibarua, na Giacinta Nannetti aliyetokea familia tajiri lakini alitengwa nayo alipoamua kuolewa na maskini huyo. Basda yake alizaliwa Ernista (1850).

Baba yake alifariki wakati Klelia alipokuwa na umri wa miaka 8 tu, naye akawa anamsaidia mama kupata riziki,[4] lakini pia alikazana kusali.

Akiwa na miaka 14 Klelia alijiunga na kundi la makatekista kama msaidizi, akawa mapema kiongozi wake kwa uamuzi wa paroko, padri Gaetano Guido.[5] Badala ya kukubali uchumba wa watu mbalimbali, aliendelea na maisha ya kitawa[5] hata akaanzisha jumuia mpya tarehe 1 Mei 1868, alipokuwa na miaka 21 tu.

Miaka miwili baadaye akafa kutokana na kifua kikuu tarehe 13 Julai 1870.

Kwa sasa masista wake 294 wanaishi katika jumuia 36 nchini Italia, India, Tanzania na Brazil.

Sauti yake

[hariri | hariri chanzo]

Mwaka mmoja baada ya kifo chake, lilianza kutokea jambo la pekee sana ambalo linadumu hata leo, yaani watu kusikia sauti yake wakati wa sala za pamoja katika jumuia za masista wake, kufuatana na lugha zao, kikiwemo Kiswahili.[6][7] Watu wengi na wenye misimamo mbalimbali waliisikia na kusema ni "tofauti na yoyote duniani".[8]

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]
  1. https://www.santiebeati.it/dettaglio/62350
  2. "Clelia Barbieri". Vatican City. Iliwekwa mnamo 2008-03-22.
  3. Martyrologium Romanum
  4. Ball, p. 52
  5. 5.0 5.1 Ball, p. 53
  6. Ball, p 51
  7. Cruz, p252
  8. Cruz, p253
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.