Bungo mbawa-nusu

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bungo mbawa-nusu
Nzi wa Nairobi (Paederus littoralis)
Nzi wa Nairobi (Paederus littoralis)
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Arthropoda (Wanyama wenye miguu yenye viungo)
Nusufaila: Hexapoda (Wanyama wenye miguu sita)
Ngeli: Insecta (Wadudu)
Ngeli ya chini: Pterygota (Wadudu wenye mabawa)
Oda: Coleoptera (Wadudu wenye mabawa magumu)
Nusuoda: Polyphaga
Familia ya juu: Staphylinoidea
Familia: Staphylinidae
Latreille, 1802
Ngazi za chini

Nusufamilia 35, 4 katika Afrika ya Mashariki:

Bungo mbawa-nusu ni mbawakawa wa familia Staphylinidae katika nusuoda Polyphaga ya oda Coleoptera walio na mabawa mafupi ya mbele. Yale ya nyuma hukunjwa chini yale ya mbele. Mwana mashuhuri wa familia hiyo ni nzi wa Nairobi (Paederus sabaeus). Ni kikundi kikubwa cha pili, baada ya Curculionidae (fukusi), chenye spishi 63.000 duniani kote. Idadi ya spishi ya Afrika ya Mashariki haijahesabiwa.

Maelezo[hariri | hariri chanzo]

Bungo hao wengi ni wadogo, hadi chini ya mm 1, lakini wengi ni mm 2-8. Kuna spishi kubwa hadi mm 35. Sifa yao bainifu ni mabawa magumu ya mbele (elitro) yaliyo mafupi sana hivi kwamba zaidi ya nusu ya pingili za nyuma za fumbatio zinaonekana. Kwa sababu ya hiyo hawafanani sana na mbawakawa na spishi kadhaa zinaweza kupotoshwa na wadudu-koleo. Baadhi ya bungo hao haruki angani, lakini takriban wote wana mabawa ya nyuma, yanayokunjwa chini ya yale ya mbele ili kuyakinga.

Mwili ni mrefu na mwembamba, ingawa spishi kadhaa zina umbo la duaradufu. Vipapasio vina umbo la nyuzi na kuwa na pingili 11. Rangi zinaweza kuwa njano, nyekundu, kahawianyekundu, kahawia na nyeusi, hata buluu na kijani zinazong'aa.

Lava wanafanana na wapevu bila mabawa na mara nyingi wenye mandibulo ndefu. Lava wachana ni kama viwavi wadogo.

Biolojia na ekolojia[hariri | hariri chanzo]

Bungo mbawa-nusu wanajulikana kutoka karibu kila aina ya makazi na lishe yao inajumuisha karibu kila kitu isipokuwa tishu hai za mimea ya juu, ingawa angalau spishi moja huila. Wengi wao ni mbuai wa wadudu na vertebrata wengine wakiishi kwenye takataka za majani za misitu na mimea inayooza kama hizo. Pia hupatikana kwa kawaida chini ya mawe na karibu na kingo za maji matamu. Takriban spishi 400 zinajulikana kuishi kwenye ntimbi za bahari ambazo huzama na maji kujaa[1] including the pictured rove beetle,[2]. Spishi nyingine zimezoea kuishi katika makoloni ya sisimizi na mchwa, na baadhi huishi katika uhusiano wa kufaidiana na mamalia ambapo hula viroboto na vidusia vingine, ambayo humnufaisha mwenyeji. Idadi ya spishi, haswa zile za jenasi Aleochara, ni matopasi na walamizoga, au ni vidusia wa wadudu wengine, hasa wa mabundo ya nzi fulani.

Ingawa hamu ya bungo mbawa-nusu kwa wadudu wengine ingeonekana kuwafanya kuwa watahiniwa dhahiri wa udhibiti wa kibiolojia wa waharibifu, majaribio ya kuwatumia hayajafaulu haswa. Mafanikio makubwa zaidi yanaonekana na spishi za Aleochara zilizo vidusia.

Spishi zilizochaguliwa za Afrika ya Mashariki[hariri | hariri chanzo]

  • Aleochara kenyasinuosa
  • Hasumius spp.
  • Paederus eximius
  • Paederus sabaeus
  • Philonthus carpenteri
  • Philonthus chloropterus
  • Philonthus flavicauda
  • Philonthus morio
  • Platydracus spp.

Picha[hariri | hariri chanzo]

  1. J.H. Frank & K.-J. Ahn (2011). "Coastal Staphylinidae (Coleoptera): A worldwide checklist, biogeography and natural history". ZooKeys (107): 1–98. PMC 3392188. PMID 22792029. doi:10.3897/zookeys.107.1651.  Unknown parameter |doi-access= ignored (help)
  2. P. C. Craig (1970). "The behavior and distribution of the intertidal sand beetle, Thinopinus pictus (Coleoptera: Staphylinidae)". Ecology 51 (6): 1012–1017. JSTOR 1933627. doi:10.2307/1933627.