Bundi (Tytonidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bundi
Bundi-mbuga
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Strigiformes (Ndege kama bundi)
Familia: Tytonidae (Ndege walio na mnasaba na bundi)
Jenasi: Phodilus I. Geoffroy Saint-Hilaire, 1830

Tyto Ridgway, 1914

Spishi: Angalia katiba

Bundi (pia mabundi) ni ndege mbuai wa familia Tytonidae na jenasi mbalimbali ya familia Strigidae. Ukurasa huu unahusu familia Tytonidae. Spishi hizi zina rangi ya kahawa nyuma na nyeupe mbele pamoja na madoa madogo meusi. Kichwa chao kina umbo la mviringo na uso mwao una umbo la moyo. Bundi hula ndege na wanyama wadogo, wanyama wagugunaji hasa, lakini wadudu wakubwa pia. Jike huyataga mayai 2-7 kwa mahali palipofunika kama tago lililoachwa na ndege mwingine ndani ya tundu ya mti, ufa wa mwamba, dari la nyumba au kihenge n.k.

Mwenendo[hariri | hariri chanzo]

Bundi huwinda usiku na hupumzika mchana. Wanamlenga mbuawa wao kwa msaada ya masikio yao. Manyoya ya uso yapeleka mawimbisauti kwa vipenyo vya masikio viliopo mahali tofauti kidogo kimoja kuliko kingine. Hivyo wanaweza kumkamata mbuawa bila kumwona. Mbuawa hawezi kumsikia bundi akija, kwa sababu mabawa ya bundi hayafanyi sauti yo yote kwa kuwa kingo ya mbele ya manyoya ya mabawa imekerezekakerezeka na ile ya nyuma ina matamvua. Hii inapunguza vurugu ya hewa na kwa hivyo uvumi.

Msambao[hariri | hariri chanzo]

Familia hii inayosambaa kwenye eneo pana, ingawa haipo katika kaskazini mwa Amerika ya Kaskazini, Sahara ya Afrika na maeneo makubwa ya Asia. Wanaishi katika makazi mengi kutoka jangwa hadi misitu na kutoka kanda za wastani hadi za tropiki. Nyingi za spishi ishirini zilizopo bado za bundi hazijulikani sana. Baadhi, kama bundi mwekundu, wameonekana kwa nadra au kutafitiwa kidogo tu tangu uvumbuzi wao, kinyume na bundi-mabanda ambaye ni mojawapo ya spishi maarufu za bundi duniani. Hata hivyo, nususpishi kadhaa za bundi-mabanda hustahili kuwa spishi tofauti, lakini hazijulikani sana.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]


Spishi za kabla ya historia[hariri | hariri chanzo]

Picha[hariri | hariri chanzo]