Wimbisauti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wimbisauti (au: wimbi la sauti) ni njia ya uenezaji wa sauti katika nafasi.

Kwa macho ya fizikia "sauti" ni mtetemo wa gimba (kwa mfano utando) unaoendelea kama wimbi katika midia ulipo. Kwa macho ya fiziolojia na saikolojia "sauti" ni mapokezi ya wimbisauti kwa milango ya fahamu hasa sikio na utambuzi wake katika ubongo.

Wimbisauti na midia[hariri | hariri chanzo]

Wimbisauti ni wimbi mekanika yaani inahitaji midia inapoenea. Haiwezi kuenea katika ombwe. Kimsingi ni wimbi la shinikizo lililosababishwa na mtetemo wa gimba asilia halafu mtetemo huu unaendelea katika midia kama ufuatano wa vipindi vifupi vya shinikizo juu na duni katika

  • gesi, kwa mfano hewa: mtetemo katika kikoromeo shingoni unatikisisha hewa na kutoka nje kupitia hewa ya nafasi tuliko
  • kiowevu, kwa mfano maji: kama chuma inagongwa kwa nyundo chini ya maji mtetemo wake unaendelea katika maji; mtu mwenye kichwa chini ya maji anasikia sauti hii. Nyangumi wanawasiliana kwa kuimba chini ya maji, mtetemo wa sauti ao unasafiri kwa njia ya mawimbi ya shinikizo ndani ya maji.
  • dutu mango, kwa mfano gimba la metali: kama bomba ndefu inagongwa sauti yake inasikika kwa kuweka sikio moja kwa moja juu ya bomba hata kwa umbali mkubwa.

Kasi ya wimbisauti ni tofauti kutegemeana na midia inapopita.

  • ndani ya hewa yenye sentigredi 20 sauti inatembea mita 343 kwa sekunde, yaani kilomita 1 kwa sekunde 3, au takriban kilomita 20 kila dakika.
  • ndani ya maji ya bahari sauti inatembea mita 1,500 kwa sekunde, hivyo takriban kilomita 90 kila dakika.
  • ndani ya gimba la chuma sauti inatembea mita 5160 kwa sekunde, hivyo takriban kilomita 300 kila dakika (kama bomba au pau ndefu vile ya chuma ipo)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]

Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
Wikimedia Commons ina media kuhusu:

Kigezo:Library resources box