Bundi (Strigidae)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Bundi
Bundi masikio-mafupi
Uainishaji wa kisayansi
Himaya: Animalia (Wanyama)
Faila: Chordata (Wanyama wenye ugwe wa neva mgongoni)
Ngeli: Aves (Ndege)
Oda: Strigiformes (Ndege kama bundi)
Familia: Strigidae (Ndege walio na mnasaba na bundi)
Nusufamilia: Asioninae (pamoja na jenasi moja ya Striginae)
Ngazi za chini

Jenasi 3 (pamoja na 1 ya Striginae):
Asio Brisson, 1760
Nesasio J.L. Peters, 1937
Pseudoscops Kaup, 1848
Strix (Striginae) Linnaeus, 1758

Bundi (pia mabundi) ni ndege mbuai wa familia Tytonidae na jenasi mbalimbali ya familia Strigidae. Ukurasa huu unahusu familia Strigidae. Spishi hizi zinaainishwa katika nusufamilia Asioninae na jenasi moja ya nusufamilia Striginae.

Bundi hawa wana kichwa kikubwa chenye umbo la mviringo, mkia mfupi na rangi ya kamafleji. Kwa kawaida jike ni mkubwa kuliko dume. Mabawa yao ni marefu na mapana. Hula ndege na wanyama wadogo, wanyama wagugunaji hasa, lakini watambaachi na wadudu wakubwa pia. Jike huyataga mayai 2-7 katika tundu la mti au tago lililoachwa na ndege mwingine, pengine katika sanduku la kutagia.

Bundi wengi huwinda usiku na hupumzika mchana. Wanamlenga mbuawa wao kwa msaada ya masikio yao. Manyoya ya uso yapeleka mawimbisauti kwa vipenyo vya masikio ambavyo kimoja kipo juu kidogo kuliko kingine. Hivyo wanaweza kumkamata mbuawa bila kumwona. Mbuawa hawezi kumsikia bundi akija, kwa sababu mabawa ya bundi hayafanyi sauti yo yote kwa kuwa kingo ya mbele ya manyoya ya mabawa imekerezekakerezeka na ile ya nyuma ina matamvua. Hii inapunguza vurugu ya hewa na kwa hivyo uvumi.

Spishi za Afrika[hariri | hariri chanzo]

Spishi za mabara mengine[hariri | hariri chanzo]

Spishi ya kabla ya historia[hariri | hariri chanzo]

  • Asio brevipes (Mwisho wa Pliocene ya Hagerman, MMA)
  • Asio priscus (Mwisho wa Pliocene ya Kisiwa cha Santa Rosa, MMA)
  • Strix brea (mwisho wa Pleistocene ya Amerika ya Kaskazini)
  • Strix dakota (mwanzo wa Miocene ya South Dakota, MMA) – labda haistahili kuwa katika jenasi Strix
  • Strix edwardsi (kati ya Miocene ya Grive-Saint-Alban, Ufaransa) – labda yastahili kuwa katika jenasi Ninox
  • Strix ignota (kati ya Miocene ya Sansan, Ufaransa) – labda haistahili kuwa katika jenasi Strix
  • Strix intermedia (mwanzo – kati ya Pleistocene ya Ulaya ya Kati) – labda ni spishi ndogo ya S. Aluco ambayo imekwisha sasa
  • Strix wintershofensis (mwanzo – kati ya Miocene ya Wintershof, Ujerumani wa Magharibi) – labda yastahili kuwa katika jenasi Ninox
  • Strix sp. (mwisho wa Miocene ya Nebraska, MMA)
  • Strix sp. (mwisho wa Pliocene ya Rębielice Królewski, Poland)
  • Strix sp. (mwisho wa Pleistocene ya Ladds, MMA)

Picha[hariri | hariri chanzo]