Azimio la Arusha
Azimio la Arusha ni tamko rasmi la kisiasa lilikosudiwa kuongoza Tanzania katika njia ya ujamaa kadiri ya maelekezo hasa ya Julius Kambarage Nyerere.
Jina la azimio linatokana na mji wa Arusha lilipitishwa tarehe 26-29 Januari 1967.
Tarehe 5 Februari 1967 Mwalimu Nyerere alilitangaza huko Dar es Salaam kama uamuzi wa Watanzania wa kuondoa unyonge wao.
Tamko la Arusha lina sehemu tano: Itikadi ya chama cha TANU; Siasa ya ujamaa; Siasa ya kujitegemea; Uanachama wa TANU; na Azimio la Arusha.
Kiini chake ni hiki: "Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwa. Sasa tunataka mapinduzi, mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na tusipuuzwe tena".
Hati yenyewe kwa Kiingereza
- TANU, Dar es Salaam. (1967). The Arusha Declaration and TANU’s Policy on Socialism and Self Reliance. Dar es Salaam:Tanzania. Published by the Publicity Section, TANU, Dar es Salaam.
- Text of Arusha Declaration (engl.)
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |