Nenda kwa yaliyomo

Azimio la Arusha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mnara wa Uhuru, Arusha.

Azimio la Arusha ni tamko rasmi la kisiasa lililokusudiwa kuongoza Tanzania katika njia ya ujamaa, ikifuata maelekezo ya kiongozi wa Taifa, Julius Kambarage Nyerere.[1][2][3]

Jina la azimio linatokana na mji wa Arusha, na tamko hili lilipitishwa kati ya tarehe 26 hadi 29 Januari 1967. Baada ya hapo, tarehe 5 Februari 1967, Mwalimu Nyerere alilitangaza rasmi huko Dar es Salaam kama uamuzi wa Watanzania wa kuondoa unyonge wao.[4][5]

Azimio la Arusha lina sehemu tano kuu:

  1. Itikadi ya chama cha TANU
  2. Siasa ya ujamaa
  3. Siasa ya kujitegemea
  4. Uanachama wa TANU
  5. Azimio la Arusha

Kiini cha azimio kilielezwa kwa maneno haya:

"Tumeonewa kiasi cha kutosha, tumenyonywa kiasi cha kutosha, tumepuuzwa kiasi cha kutosha. Unyonge wetu ndio uliotufanya tuonewe, tunyonywe na kupuuzwe. Sasa tunataka mapinduzi—mapinduzi ya kuondoa unyonge ili tusionewe tena, tusinyonywe tena na tusipuuzwe tena."

Hati yenyewe kwa Kiingereza

  • TANU, Dar es Salaam. (1967). The Arusha Declaration and TANU’s Policy on Socialism and Self Reliance. Dar es Salaam:Tanzania. Published by the Publicity Section, TANU, Dar es Salaam.[6]
  • Text of Arusha Declaration (engl.)

Tanbihi

  1. Rwekaza, S. (2008). "The Arusha Declaration and Tanzanian Socialism". *Tanzania Journal of Historical Studies*, 10(2), 21–35.
  2. Pratt, C. (1999). *Politics and Development in Tanzania*. London: Routledge. pp. 45–50. ISBN 978-0-415-19112-1.
  3. Nyerere, J.K. (1967). "Azimio la Arusha". Arusha Declaration. Dar es Salaam: Government Printer.
  4. Vaughan, M. (2011). *Nyerere and the Emergence of Socialism in Tanzania, 1960–1967*. Cambridge: Cambridge University Press. ISBN 978-1-107-00516-5.
  5. Iliffe, J. (1979). *A Modern History of Tanganyika*. Cambridge University Press. pp. 364–370. ISBN 978-0-521-29464-1.
  6. "[The Arusha Declaration]". 1967. {{cite journal}}: Cite journal requires |journal= (help)
Makala hii kuhusu mambo ya siasa bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Azimio la Arusha Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Historia ya Tanzania
Coat of Arms of Tanzania
This article is part of a series
Uendo
Historia ya Zanzibar
Afrika Mashariki 1800-1845
Ukoloni
Afrika ya Mashariki ya Kijerumani
Mkataba wa Zanzibar-Helgoland
Mkwawa
Vita vya Maji Maji
Vita vikuu vya kwanza Afrika Mashariki
Tanganyika
Mapambano ya uhuru Tanganyika
Uhuru
Uhuru wa Tanganyika
Mapinduzi ya Zanzibar
Muungano wa Tanganyika na Zanzibar
Julius Nyerere
Ujamaa
Tamko la Arusha
Vita vya Kagera
Ali Hassan Mwinyi
Benjamin Mkapa
Jakaya Kikwete
John Magufuli
Samia Suluhu Hassan

Tanzania Portal