Nenda kwa yaliyomo

Agnes wa Praha

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Agnesi wa Praha)
Mt. Agnes akiuguza wagonjwa, sehemu ya mchoro wa karne XV.

Agnes wa Praha (au wa Bohemia) alizaliwa Praha (leo mji mkuu wa Ucheki) mwaka 1211 akafariki huko tarehe 2 Machi 1282).

Mwanzilishi na abesi wa monasteri ya Mt. Fransisko mjini Praha, alianzisha pia Shirika la Wanamsalaba wa Nyota Nyekundu.

Anaheshimiwa na Kanisa Katoliki kama mtakatifu bikira, hasa katika tarehe ya kifo chake[1] au tarehe 6 Machi.

Binti wa mfalme wa Bohemia Ottokar I na Kostanza wa Hungaria, alikuwa ndugu wa jirani wa watakatifu Ludmila, Venseslaus, Edwiga, Elizabeti wa Hungaria na Margerita wa Hungaria.

Kisha kulelewa katika monasteri ya masista wa Citeaux huko Trzebnica, na ya masista wa Premontree huko Doksany, alipokuwa na miaka 8 alitumwa kwenye ikulu ya Vienna ili kuandaliwa awe mke wa kaisari Henri VII wa Ujerumani, mwana wa Federiko II.

Akiguswa na mfano wa Fransisko wa Asizi, aliamua kuishi kitawa na kwa msaada wa Papa Gregori IX alivunja uchumba wake akarudi Praha awe bibiarusi wa Kristo tu.

Huko alianzisha konventi ya kwanza ya Ndugu Wadogo katika eneo hilo(1232), ikiwa pamoja na hospitali kwa mafukara: ili kuendesha hospitali hiyo alianzisha chama cha kitume cha Wanamsalaba ambao mwaka 1237 walikubaliwa na Papa kuwa shirika la kitawa.

Mwaka 1234 alianzisha monasteri ya Waklara iliyopokea masista watano waliotumwa na Klara wa Asizi mwenyewe: Agnes alihamia huko tarehe 11 Juni mwaka huohuo akishika kikamilifu ufukara mkuu. Baadaye akawa abesi wake hadi kifo chake.

Heshima baada ya kifo

[hariri | hariri chanzo]

Agnes aliheshimiwa sana mara baada ya kufa: tarehe 28 Novemba 1874 Papa Pius IX alithibitisha heshima hiyo na jina alilopewa la mwenye heri. Tarehe 12 Novemba 1989 Papa Yohane Paulo II alimtangaza mtakatifu.

Tazama pia

[hariri | hariri chanzo]

Marejeo mengine

[hariri | hariri chanzo]
  • Seton, Walter W. Some New Sources for the Life of Blessed Agnes of Bohemia: Including a Fourteenth-Century Latin Version. Cambridge: Cambridge University Press (2010). ISBN 1108017606

Viungo vya nje

[hariri | hariri chanzo]
Wikimedia Commons ina media kuhusu:
Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.