Yohane Southworth

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mt. Yohane Southworth katika mavazi ya ibada.

Yohane Southworth (Lancashire, Uingereza, 1592 hivi – Tyburn, London, 28 Juni 1654) alikuwa Mkristo wa Kanisa Katoliki pamoja na familia yake wakati wa dhuluma ya nchi hiyo iliyotaka wote wawe Waanglikana[1].

Baada ya kuhamia Ufaransa, aliingia seminari kwa kengo la kurudi kwao kufanya uchungaji usioruhusiwa na serikali. Kisha kupewa daraja ya upadri alifaulu kufanya utume Uingereza miaka 1619-1624[2] na 1626-1627[3].

Ndipo alipokamatwa na kukaa gerezani hadi mwaka 1630 alipofukuzwa nchini badala ya kuuawa kama alivyohukumiwa.

Mwaka 1636 alikuwa amerudi London akawa anahudumia wagonjwa wa tauni[4]. Kati ya miaka 1637 na 1640 mra nne alikamatwa na kuachwa au kutoroka akiendelea na utume kwa siri hadi mwaka 1654 aliponyongwa na kukatwakatwa chini ya sheria.

Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri mwaka 1929. Halafu Papa Paulo VI tarehe 25 Oktoba 1970 akamtangaza kuwa mtakatifu mfiadini pamoja na wenzake 39.

Sikukuu yake ni tarehe 28 Juni[5].

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Christian cross.svg Makala hii bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.