Yohane Baptista de La Salle
Yohane Baptista de la Salle (kwa Kifaransa: Jean-Baptiste de La Salle; Reims, Ufaransa, 30 Aprili 1651 - Saint-Yon, Rouen, Ufaransa, 7 Aprili 1719) alikuwa padri wa Kanisa Katoliki na mlezi wa vijana wengi, hasa fukara, ambaye kwa ajili ya malezi yao ya kiutu na ya Kikristo alianzisha pia kwa tabu nyingi shirika la Mabradha wa Shule za Kikristo[1].
Anahesabiwa mwanzilishi wa shule Katoliki duniani. De La Salle anahesabiwa pia kuwa wa kwanza kuendesha chuo cha ualimu (1685).
Anaheshimiwa kama mtakatifu na msimamizi wa walimu.
Sikukuu inaadhimishwa kila tarehe 7 Aprili[2] au 15 Mei.
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Akifuata njia ya upadri tangu utotoni, alimaliza masomo na kupata upadirisho tarehe 9 Aprili 1678.
Miaka miwili baadaye alipata udaktari wa teolojia.
De La Salle aliingia kazi ya malezi taratibu, bila ya kukusudia, kadiri ya matukio na watu aliokutana nao.
Juhudi zake za kuanzisha shirika la mabradha tu kwa ajili ya kuendesha shule zilipata upinzani mkubwa kwa sababu ulikuwa mpango mpya.
Pia mbinu zake zilikuwa hazijazoeleka, kama vile kutumia lugha ya kawaida na kutodai ada yoyote.
Hata hivyo alifaulu kuanzisha mtandao wa shule nchini Ufaransa.
Heshima baada ya kifo
[hariri | hariri chanzo]Alitangazwa na Papa Leo XIII kuwa mwenye heri tarehe 19 Februari 1888 na mtakatifu tarehe 24 Mei 1900.
Papa Pius XII alimtangaza msimamizi wa walimu wote tarehe 15 Mei 1950.
Athari yake
[hariri | hariri chanzo]Kazi yake ilienea haraka. Leo duniani shirika lake lina mabradha 2,883 (mbali ya walei na watawa zaidi ya 100,000 wanaoshiriki kazi yao) wanaolea vijana kama 1,160,000 katika vituo vya malezi 1,154 vya nchi 78.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Complete works of St John Baptist de La Salle Ilihifadhiwa 7 Agosti 2010 kwenye Wayback Machine. PDF format
- De La Salle Christian Brothers worldwide official website
- The Vocation of the Brothers United States & Canada
- Compendium of Lasallian Resources Ilihifadhiwa 30 Oktoba 2016 kwenye Wayback Machine.
- Founder Statue in St Peter's Basilica
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |