Yoana Antida Thouret
Yoana Antida Thouret (kwa Kifaransa: Jeanne Antide; Sancey-le-Long, Ufaransa, 27 Novemba 1765 - Napoli, Italia, 24 Agosti 1826) alikuwa mtawa wa Kanisa Katoliki aliyeanzisha shirika la Masista wa Upendo wa Kimungu kwa ajili ya malezi ya Kikristo na ya kiraia ya vijana na matendo ya huruma kwa watoto wasio na familia, kwa fukara na kwa wagonjwa[1].
Anaheshimiwa kama mtakatifu bikira.
Sikukuu yake inaadhimishwa kila mwaka tarehe ya kifo chake[2].
Maisha
[hariri | hariri chanzo]Yoana Antida alizaliwa Sancey-le-Long tarehe 27 Novemba 1765.
Alipofikia umri wa miaka 22 alijiunga na Masista wa Huruma wa mt. Vinsenti wa Paulo huko Paris, lakini wakati wa Mapinduzi ya Kifaransa aliishi uhamishoni Uswisi na Ujerumani, baada ya kulazimika kuacha shirika mwaka 1789.
Mwaka 1797 alirudi Ufaransa alipoanzisha shule kwa wasichana fukara.
Mwaka 1799 alianzisha shirika lingine huko Besançon, kwa msaada wa Letizia Ramolino, mama wa Napoleon Bonaparte. Shirika jipya lilienea haraka hata nje ya Ufaransa, katika nchi za Savoy, Uswisi na Italia.
Mwaka 1819, shirika lake lilikubaliwa na Papa Pius VII na kupewa fadhili ya kutokuwa chini ya askofu wa jimbo. Hiyo ilisababisha upinzani wa askofu wa Besançon, Gabriel Cortois de Pressigny, mwenye mwelekeo wa Ugalikani.
Hivyo Yoana alihamia Italia, alikofariki katika monasteri Regina Coeli, Napoli, tarehe 24 Agosti 1826, akiwa ameishiwa nguvu kutokana na mateso makubwa yaliyomuandama.
Heshima baada ya kufa
[hariri | hariri chanzo]Kufuatana na sifa ya utakatifu wake iliyozidi kuenea, Papa Pius XI alimtangaza mwenye heri tarehe 23 Mei 1926, halafu mtakatifu tarehe 14 Januari 1934.
Tazama pia
[hariri | hariri chanzo]- Watakatifu wa Agano la Kale
- Orodha ya Watakatifu Wakristo
- Orodha ya Watakatifu wa Afrika
- Orodha ya Watakatifu Wafransisko
Tanbihi
[hariri | hariri chanzo]Marejeo
[hariri | hariri chanzo]- Bernard Paul, La bienheureuse Jeanne-Anthide Thouret, fondatrice de la congrégation des Soeurs de la Charité de Besançon et de Naples, 1926.
Viungo vya nje
[hariri | hariri chanzo]- Shirika la Mt. Vinsenti wa Paulo Ilihifadhiwa 2 Oktoba 2009 kwenye Wayback Machine.
- Tovuti ya shirika yenye maisha ya Jeanne-Antide Thouret
- Maisha Ilihifadhiwa 9 Novemba 2010 kwenye Wayback Machine.
Makala hii bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Mkristo huyu, kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Je, unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari. |